BENKI ya CRDB, imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu
ya Kamati ya Amani na ushirikiano ikiwa ni maandalizi ya mechi baina ya
viongozi wa madhehebu ya dini.
Mtanange wa viongozi hao unatarajiwa kufanyika Oktoba 12,
mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha siku
ya amani duniani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi na hundi ya sh.
milioni tano ikiwa ni maadhimisho ya
wiki ya wateja, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema muungano huo
umeonyesha sura ya kushirikiana baina ya madhehebu mbalimbali.
“Nchi mbalimbali zimechafuka kwasababu ya migogoro ya dini,
lakini viongozi hawa wameonyesha muungano na sisi wengine tunapaswa
kushirikiana na kuvuruga amani kwa imani za dini zetu,”alisema.
Dk. Kimei alivitaja vifaa hivyo ni jezi zenye rangi mbili
tofauti, tracksuit ambapo kila jezi zikiwa 40, na kuwapatia hindi y ash.
milioni tano kwaajili ya maandalizi.
Aidha alisema CRDB itaendelea kuwa karibu na wateja wake
ili kushirikiana nao na kuendeleza huduma.
Mtanange huo utawajumisha Masheikh, Maimamu, Maaskofu, Wachungaji
na Mapadre huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Naye Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi
ya mchezo huo aliishukuru benki hiyo na
kueleza kuwa lengo la mchezo huo ni kuimarisha amani iendelee kudumu.
Naye Katibu Padre John Solomon, alisema kuwa wameamua
kuonyesha mchango wa kuthamini amani na kuepuka mapigano.
Viongozi hao wa dini wameshaanza mazoezi kwajili ya
kujiweka tayari kufanya vizuri katika mchezo huo wa kuhamasisha amani na utulivu
nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei (wa
tatu kushoto) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya michezo Mwenyekiti wa Kamati ya
Amani ya Viongozi wa Dini, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad
Mussa Salum kwa ajili ya mechi ya viongozi wa Kamati ya Amani na Ushirikiano
inayowaunganisha viongozi wa dini zote itakayofanyika Oktoba 12 kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa
Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, Katibu wa Kamati hiyo, Padri John Solomon (wa pili
kulia), Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya
Kijitonyama, Lucas Busigazi (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mchungaji George Fupe (wa pili kushoto).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles kimei akizungumza na waandishi wa habari.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akionyesha jezi namba 9 atakayoitumia katika mchezo huo.
Dk. Kimei akifurahia jambo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa viongozi wa timu ya Kamati ya Amani na ushirikiano ikiwa ni maandalizi ya mechi baina ya viongozi wa madhehebu ya dini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akitoa ufafanuuzi kwa mteja wa Benki ya CRDB kuhusu huduma mbalimbali za benki hiyo. Dk. Kimei alijumuika na wafanyakazi wa tawi la Kijitonyama katika kuwahudumia wateja wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya wateja wa Benki hiyo inayoanza Oktoba 6.
Baadhi yawateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.
Baadhi yawateja wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kupata huduma katika tawi la Kijitonyama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akigonga muhuri katika cheki ya mteja.
Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwa na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Silvia Lupembe.
Dk. Kimei akitoa ufafanuazi kwa mmoja wa wateja waliofika katika tawi la Benki ya CRDB Kijitonyama kupata huduma.
Dk. Kimei akimsikiliza mteja wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama.
Wateja wakipata huduma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akijaza fomu ya kufungua akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya mtoto Daud Stephen (6) (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki iliyoanza jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto) akijaza fomu ya kufungua akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya mtoto Daud Stephen (6) (katikati) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki iliyoanza jijini Dar es Salaam.
Keki iliyopambwa vizuri ikisubiri kukatwa kwa ajili wateja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akikata keki ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Mteja mdogo kuliko wote wa tawi la Kijitonyama, Daud Mwakwenda (6) akilishwa keki na Dk. Kimei wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Maxcom, Juma Rajabu akilishwa keki na Dk. Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akimkabidhi maua mteja wa Benki ya CRDB aliyefika katika tawi la Kijitonyama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Benki ya CRDB na maofisa wa benki hiyo.
No comments:
Post a Comment