Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba wakati wa mkutano wa mwaka wa wachumi na
maafisa mipango unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na
maafisa mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga akizungumza na washiriki wa
Mkutano huo kabla ya kuufungua rasmi.
Baadhi ya viongozi wa wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani). Kutoka Kushoto ni Naibu Katibu
Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara, anayemfuatia ni Bw. Paul
Sangawe (Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na
Mahusiano ya Kiuchumi) na Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na
Masuala ya Idadi ya Watu) Bibi Florence Mwanri.
Washiriki
wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).
Washiriki wa mkutano wa mwaka wa wachumi na
maafisa mipango wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Balozi Dkt. Matern
Lumbanga (katikati waliokaa) pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango.
Washiriki
wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango wakimsikiliza Katibu Mtendaji
wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Hayupo pichani).
Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia)
akimpongeza na kumshukuru Mgeni Rasmi wa mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa
mipango, Balozi Dkt. Matern Lumbanga mara baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
picha ya pamoja.
Picha na SAIDI MKABAKULI
Picha na SAIDI MKABAKULI
========== ======= ===========
Mkutano wa kitaalamu ambao unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka
tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia
uchumi na mipango umefunguliwa rasmi na Balozi (Mstaafu) Dkt. Matern Lumbanga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi (Mstaafu)
Dkt. Lumbanga alisema kuwa wachumi
na maafisa mipango wana wajibu mkubwa katika kuishauri serikali juu ya njia bora
na madhubuti za kupambana na umaskini na kuharakisha maendeleo kwa jamii ya
Watanzania.
“Muna dhima kubwa katika
kushauri kitaalamu juu ya namna nzuri za kupunguza tatizo sugu la umaskini
miongoni mwa Watanzania,” alisema.Balozi (Mstaafu) Dkt. Lumbanga aliwasihi washiriki kutumia fursa hiyo kujadili kwa
kina na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala
ya maendeleo ya kitaaluma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Katibu
Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema kuwa
lengo kuu la mkutano huo ni kutoa
fursa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu
ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Aliongeza kuwa Mkutano huo, unatoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu
ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na
ujuzi kwenye masuala hayo.
“Mkutano huu ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa
minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini,”
alisema Dkt. Mpango. Kwa mujibu wa ratiba ya mkutano huo, Mada mbalimbali zinawasilishwa kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya
kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, ambapo mkutano huo unajadili masuala ya Maendeleo
ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu) na Maandalizi
ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021).
Mada nyingine ni pamoja na Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji
katika Sekta ya Umma ambao una lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na
uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya
miradi na program za maendeleo. Pamoja na mada ya Namna bora ya kujiandaa na
Uchumi wa Gesi.
Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na
mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na
wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti
wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.
No comments:
Post a Comment