Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi wiki ya
Rasilimali watu itakayowawezesha wafanyakazi wake kupata elimu kuhusu
Sera na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wafanyakazi na kusimamiwa
na kitengo cha Rasillimali watu kwa lengo la kuwaongezea wafanyakazi
ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja.
Airtel imeandaa wiki hiyo ya rasilimali watu katika nchini zote Afrika
ambapo Airtel inafanya biashara zake na kuzinduliwa rasmi leo nchi
Tanzania, airtel imefanya hivyo leo ikiwa ni muda mfupi tu tangu
ilipoadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa duniani kote
ambapo airtel ilishiriki katika maadhimisho hayo .
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa kitengo cha Rasilimali
watu Bwana Patrick Foya alisema” Tunategemea kuwa na wiki yenye
mafanikio ambayo itawawezesha wafanyakazi wetu kupata ufafanuzi juu ya
maswala mbalimbali yanayohusu sera na haki zao za msingi kama
wafanyakazi wa Airtel.
Sambamba na hilo tutakuwa na watoa huduma
kutoka kwenye makampuni mengine wakiwemo strategies inayotoa huduma za
bima ya afya, NSSF inayotoa mikopo ya nyumba na mafao kwa wafanyakazi
na makapuni mengine mengi ambayo yatatoa fulsa ya wafanyakazi wetu
kupata elimu zaidi kuhusu huduma hizi muhimu na jinsi yakufaidika nazo
hii ni fulsa kwa wafanyakazi wetu nasi tuko tayari kuwafikishia wote
ili kuongeza ufanisi kazini".
Natoa wito kwa wafanyakazi kujitokeza katika sehemu maalumu
zilizoandaliwa kutoa huduma na kupata mambo mazuri tuliyowaandalia
wiki nzima alingoza Foya.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwashukuru
wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu kwa kujipanga vyema kwa
wiki hii na kusisitiza kuwa elimu na mafunzo haya ni mwendelezo wa
mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa wafanya kazi wote wanajua mambo
muhimu yanayotokana na ajira zao, sera mbalimbali kama vile za afya na
zile zinazogusa maslahi yao'.
Colaso alisema “ natoa wito kwa wafanyakazi kutumia wiki vyema na
kuuliza mswali mengi yatakayo toa ufafanuzi wa maswala wanayohitaji
elimu na uelewa zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwn Sunil Colaso akiongea na
wafanyazi wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika
katika Ofisi za makao makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata
fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao
za kimsingi na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na
kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika
ofisi za Airtel Moroco.
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu cha Airtel
Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa wiki ya
Rasilimali watu iliyozinduliwa rasmi jana katika ofisi za makao makuu
ya Airtel jijini Dar es saalam.
wafanyakazi wa Airtel wakifatilia uzinduzi wa uzinduzi wa wiki ya
Rasilimali watu iliyozinduliwa rasmi jana katika ofisi za makao makuu
ya Airtel jijini Dar es saalam
Meneja Rasilimali watu Airtel Bi Sophia Melamari akiongea wakati wa
uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao
makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu
ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao za kimsingi na huduma
nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali watu,
hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroco.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali watu Airtel Tanzania Patric Foya
akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika
katika Ofisi za makao makuu ya Airtel ambapo wafanyakazi watapata
fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao
za kimsingi na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na
kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika
ofisi za Airtel Moroco.
Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu kama MC Pilipili akitoa burdani
kwa wafanyakazi wa Airtel wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu
iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya
sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha
Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za
Airtel Moroco.
Wafanyakazi wa Airtel wakifurahia burdani toka kwa Mchekeshaji na
mshereheshaji maarufu kama MC Pilipili wakati wa uzinduzi wa wiki ya
Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata
elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na
Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika
ofisi za Airtel Moroco.
No comments:
Post a Comment