KAMPUNI ya simu za mkononi ya airtel imezindua rasmi namba
itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya
muziki ya Airtel Trace Music Stars kwa kurekodi na kutuma nyimbo zao
kwa kutumia simu zao za mkononi huku baadhi ya wasanii chipukizi
wakipata nafasi yakuonyesha vipaji vyao katika viwanja vya Coco Beach
Akizungumza katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani mbalimbali
ikiwemo Yamoto bendi katika viwanja vya Coco beach jijini Dar es
salaam meneja uhusiano wa airtel bw. jackson mmbando amesema kila
mtanzania anayo nafasi ya kushiriki katika shindano hilo kwa kupiga
simu namba 0901002233.
Aidha Mmbando ameongeza kuwa lengo la kuanzisha shindano hilo ni
kuinua vipaji vya watanzania wenye kujua kuimba ili wapate nafasi ya
kuwa staa wa kimataifa.
Nae balozi wa shindano hilo Ommy Dimpoz amewaomba watanzania
kujitokeze kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo ambapo mshindi
atajinyakulia zawadi kabambe ikiwemo kurekodi na kusambaziwa nyimbo
zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na safari ya kwenda
nchini marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimuziki na nguli wa
muziki wa amerika Akon.
Wasanii wa kundi la yamoto band wakiwa na msanii maarufu nchini
ambae pia ni balazo wa airtel trace music stars tanzania Ommy Dimpos
wakionyesha namba maalum itakayotumika kupiga na kutuma nyimbo kwa
wasanii chipukizi kwenye shindano la airtel trace music stars
lililozinduliwa rasmi jana.
Balozi wa airtel music stars Tanzania Ommy Dimpos akitangaza
rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki mashindano ya
kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi na
kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana Coco beach.
Meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akizindua na
kutangaza rasmi namba itakayowawezesha watanzania kushiriki
mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa
kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana
coco beach.
Baadhi ya wasanii waliojitokeza wakijaribu kuimba na kurekodi
kwenye namba maalum ya kushiriki mashindano ya airtel trace music
stars katika viwanja vya coco beach ambapo airtel ilimezindua rasmi
namba ya kushirmaki shindano la airtel trace music stars kwa lengo la
kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia malengo yao ya kuwa nyota
wa musiki.
Mmoja kati ya wasanii waliojitokeza akijaribu kuimba kwenye
namba maalum ya kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Stars
katika viwanja vya coco beach huku meneja uhusiano wa airtel Jackson
Mmbando akishuhudia. Airtel imezindua mashindano haya ya Airtel Trace
Music stars kwa lengo la kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia
malengo yao.
Wasanii wa kundi maarufu na linalofanya vizuri toka TMK yamoto
band wakionyesha vitu vyao wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa namba
maalum itakayotumika kupiga na kurekodi nyimbo na wasanii chipukizi
ili kujishidia dili la kurediwa nyimbo zao marekani kupitia shindano
maalum la airtel trace music stars katika viwanja vya coco beach
jijini dar es salaam.
No comments:
Post a Comment