Monday, September 15, 2014

TASWIRA ZA MAPAMBANO MAWILI YA NGUMI MKOANI KILIMANJARO

Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama cha Ngumi mkoa wa Kilimanjaro Elikunda Kipoko wakati wa mapambano hayo 
Mapambano ya utangulizi yakaanza .
Mgeni rasmi katika mapambano mawili ya ngumi ya kimataifa ,mkuu wa wilaya ya Hai ,Novatus Makunga akizungumza wakati wa mapambano hayo kati ya Bondia Said Yazidu(Tanzania) na Djamel Dahou(Aljeria) .
Muandaaji wa Pambano hilo,Andrew George akionesha mkanda wa Ubingwa wa Afrika ulikuwa ukigombewa na Bondia Alibaba Ramadhan(Tanzania) na Aleck Mwenda(Malawi).
Mgeni rasmi ,Novatus Makunga akonesha mkanda huo kwa mashabiki.
Pambano likaanza kati ya Bondia,Alibaba(Mwenye Bukta nyekundu) na Aleck Mwenda(Mwenye Bukta nyeusi)
Alibaba akajaribu kupiga ngumi kadri alivyoweza.
Aleck Mwenda pia akajibu mapigo ingawaje yake yalionekana makali zaidi.
Bondia Mwenda alikuwa mzuri sana katika kujikinga.
Mwenda akamsukumia Alibaba ngumi za kutosha.
Alibaba akaenda chini mara kadhaa lakini alinyanyuka.
Round 10 zikamalizika uamuzi wa majaji ukingojewa. huku dalili zikionesha dhahiri ,Aleck Mwenda atakuwa ameshinda.
Akiwa amebebwa na wamalawi wenzake na kushangilia ,hakuamini alichosikia masikioni mwake baada ya mshindi kutangazwa Alibaba.
Furaha ikahamia kwa Alibaba.
Mashabiki wakaingia ulingoni kwa Bondia na Chupa za Bia.
Kamanda wa Polisi wa wilaya OCD, Deodatus Kasindo akamkabidhi mkanda Alibaba.
Alibaba akifurahia mkanda wake wa Kwanza baada ya kutangazwa Bingwa wa  Ngumi Afrika. 
Furaha ya Ushindi.
Likafuatia Pambano la Ubingwa wa Dunia Kati ya Bondia ,Djamel Dahou(Aljeria) na Said Yazidu .
Bondia Said Yazidu wa Tanzania akapanda ulingoni.
Mpambano ukaanza.
Kila mmoja akamvizia mwenzake.
Bondia Yazidu akapigwa vitasa kadhaa.
Akakaaa kwa mara ya kwanza.
Akasimama kisha akajitutumua ,akapigwa kitasa tena ,
Akakaa kwa mara nyingine.
Akasimama tena akachezea ngumi za kutosha .
Zikampeleka chini kwa mara ya tatu.
Akanyanyuka kwa Mbinde .
Ikashindikana na Bondia ,Dahou akashinda kwa KO ndani ya dakika 2 na sekunde 7 katika round ya kwanza.
Dahou akatangazwa Bingwa.
Mgeni rasmi ,mkuu wa wilaya ya Hai,Makunga akamkabidhi mkanda ,Bondia Dahou.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments: