Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na Uwezeshaji Dkk. Mary Nagu
akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka
65 tangu kuanzishwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
:
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing akigonga glasi ya
mvinyo wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa Jamhuri
ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Picha
ya Keki kwa ajili ya hafla ya maadhimisho ya miaka 65 tokea kuanzishwa
kwa Jamhuri ya Watu wa China hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Uwekezaji na Uwezeshaji) Dkt. Mary Nagu na Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing wakikata Keki wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa China nchini Tanzania Balozi Lui Youqing (katikati) akiteta jambo na
baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya kuadhimisha miaka 65 tokea
kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Afisa
anayeshughulikia masuala ya Menejimenti na Programu wa Aga Khana
Development Network Bw. Navroz Lakhani
Msanii
wa Jamhuri ya Watu wa China akicheza mchezo wa Wushu wakati wa hafla ya
kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana
jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni wakisoma vitabu wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu
kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wageni wakifuatilia michezo mbalimbali kutoka kwa wasanii wakati wa
hafla ya kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa
China jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHVUM.
======== ======== =======
Tanzania yaendelea kunufaika na uhusiano mwema ulipo baina yake na Taifa la China.
Na; Daud Manongi, WHVUM.
Hadi
kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 China imetoa msaada wa zaidi ya dola za
Kimarekani bilioni 1.943 kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya
maendeleo nchini Tanzania, ushirikiano wa kibiashara dola bilioni 3.7 na uwekezaji dola bilioni 2.5 na jumla ya makampuni 500 yamewekeza nchini Tanzania.
Haya
yamebainishwa na Waziri wa Nci ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji na
Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya miaka 65
ya toka kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China jana jijini Dar es
Salaam.
Dkt
Nagu amesema kuwa msaada huo utasaidia katika kutekeleza miradi ya
maendeleo ikiwema Bandari ya Bagamoyo, mradi wa EPZ, usambazaji wa umeme
ukanda wa Kaskazini – Mashariki, Elimu kwa njia ya mtandao,Serikali
Mtandao kwa ajili ya Zanzibar na Umeme wa upepo katika mkoa wa Singida. Aliongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutafungua njia za uchumi na kusababisha Tanzania kuwa na uchumi imara na endelevu.
“Najisikia
faraja kusema kuwama pamoja na mafanikia chanya tunayopata Tanzania
bado ina miradi mingi ambayo inahitaji msaada wa kifedha na kitaalam
kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China na ni imani kuwa wataendelea kutoa
ushirikiano katika kufanikisha miradi hiyo” Alisema Dkt. Nagu.
Kwa
upande wake Balozi wa China hapa nchini Balozi Lui Youqing amesema kuwa
nchi yake itaendelea kuisaidi Tanzania kwa kuwa kumekuwa na mahusiano
mazuri nay a muda mrefu baina ya nchi hizi mbili.
Balozi
Youqing ameongeza kuwa Tanzania inavutia wakezaji kwa kuwa na mazingira
salama ya kisiasa na kijamii ambapo anashawishika kuunganisha
wawekezaji wa China kushirikiana na wawekezaji wengine katika kupunguza
umasikini na kuleta maendeleo akitolea mfano ushirikiano katika sekta ya
majengo.
“Tanzania
ni nchi kubwa yenye maono na inayovutia zaidi kimataifa kutokana na
uimara wake katika Nyanja za siasa na uchumi jamii, imekuwa na ushawishi
wa hali ya juu katika anga za kikanda na kimataifa, hali inafanya
wawekezaji kutoka sehemu kama EU, US, Japana na kwingineko waongeze
uwekezaji, ata mimi binafsi nashawishika kuwashawishi wawekezaji wa
China kuwekeza zaidi katika nchi hii” Alisema Balozi Youqing.
China
inasherehekea miaka 65 toke kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1949, wkati
huo huo ni miaka 50 sasa tokea Taifa kuanzisha mahusiano ya kidiplomasia
kati yake na Tanzania uhusiano ambao umeasisiwa na Hayati Baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Zedong.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment