Wednesday, September 17, 2014

SIGOMBEI URAIS 2015 NKAMIA

GEDSC DIGITAL CAMERA
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni   Mbunge wa Kondoa Kusini ,akiongea na waandishi wa habari leo  jijini Arusha katika studio za redio 5 zenye makao yake makuu njiro ambapo alisema kuwa hana mpango wowote wakugombea nafasi ya Urais 2015
GEDSC DIGITAL CAMERA
Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa wanafanya mahojiano na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia leo jijini Arusha katika studio za redio 5 
GEDSC DIGITAL CAMERA
Mkurugenzi wa Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis akiwa anamsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia wakati akizungumza na waandishi wa habari kulia ni mwandishi wa chanel Ten Jamilah Omary.
GEDSC DIGITAL CAMERA
Mtangazaji wa redio 5 Mwangaza Jumanne akifanya mahojiano live na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia.
GEDSC DIGITAL CAMERA
Kulia Mwanaisha Suleiman akiwa anafanya yake ndani ya studio za redio 5 mara baada Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia alipofanya ziara kituoni hapo
GEDSC DIGITAL CAMERA
Muonekano wa studio ya Redio 5 wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akifanyiwa mahojiano hewani na mtangazaji wa kituo hicho Mwangaza Jumanne
GEDSC DIGITAL CAMERA
Meneja masoko wa Tan Communication media Bi.Sarah Keiya akiwa anasalimiana na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia 
GEDSC DIGITAL CAMERA
Mkurugenzi  wa Radio 5  Bw Robert Francis akiwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ofisini kwake mda mfupi kabla ya kuingia studio za redio hiyo
GEDSC DIGITAL CAMERA
GEDSC DIGITAL CAMERA
Katibu wa waziri Juma Nkamia Bw.Francis Songoro
GEDSC DIGITAL CAMERA
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia akiongea na baadhi ya uongozi wa kituo hicho ambapo aliwapongeza kwa kazi nzuri ya utangazaji katika kuburudisha na hata kuelimisha jamii kupitia vipindi vyao mbalimbali
GEDSC DIGITAL CAMERA
Meneja mbunifu wa redio 5 Vicky Mwokoyo wakiwa wanabadilishana mawazo na mtangazaji wa kituo cha Redio 5 Ashura Mohamed
GEDSC DIGITAL CAMERA
John Mhala wa gazeti la Habari leo akiwa na mwandishi mwenzake wa mwananchi Happy Lazaro wakiwa wanabadilishana mawazo ndani ya jengo la Redio 
GEDSC DIGITAL CAMERA
Waandishi wa habari pamoja na mkurugenzi wa kituo cha redio 5 Bw.Robert Francis  katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia,kulia ni mmiliki wa mtandao wa Jamiiblog Pamela Mollel.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia ambaye pia ni , Mbunge wa Kondoa Kusini amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea nafasi ya urais 2015 kama viongozi wengine wanavyotangaza nia huku akidai kuwa kazi yake kubwa nikuhakikisha wananchi katika jimbo lake wanapata maendeleo kupitia nafasi yake ya  ubunge.
 
Waziri Nkamia aliyasema hayo leo mara baada ya kufanya ziara fupi katika kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,ambapo alisema kuwa hajawa na ndoto ya kuwa Rais 2015.Alisema kuwa kiongozi anayestahili kuwa rais ni lazima awe na uwezo wa kuongoza na anayekubalika na watanzania na vigezo isiwe umri wa mtu.
 
''Pamoja na umri nilionao 42 sina mpango wowote wa kugombea nafasi ya Urais 2015 na umri usiwe kigezo cha kugombea uwezo wa kiongozi ni muhimu sana''alisema Nkamia.
 
Pia Waziri huyo aliipongeza kituo hicho cha redio kwa kazi nzuri ya kuburudisha na kuelimisha jamii kupitianvipindi vyake mbalimbali huku akiwataka kuandaa vipindi ambavyo vitawashirikisha wachezaji wazamani hali itakayosaidia kukuza na kuibua changamoto katika michezo(Habari Picha Pamala Mollel)

No comments: