Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.Picha na Othman Michuzi.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.
Baadhi ya Wachama na Wafuasi wa Chadema wakishangilia wakati Mwenyekiti wao akiwasili kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Palisi leo.
Kamishna wa Polisi,CP Paul Chagonja akitoa akiwataka wanachana na wafuasi wa Chadema kuondoka kwenye eneo hilo kwani hakuna sababu ya kufanya fujo.
Ulinzi mlali katika eneo hilo.
Amri ikipita ya kuwataka wanachadema kuondoka eneo hilo.
Askari akiwataka wanachadema kuondoka.
Huyu alikuwa akikaidi amri ya Jeshi la Polisi ilibidi aondolewe kwa nguvu.
Ulinzi Mkali.
Baadhi ya wanachama wa Chadema wakiondolea ndani la eneo la Makao Makuu wa Chadema.
1 comment:
CHADEMA nadhani wachunguzwe vizuri kuna sehemu wanakopata pesa za kuvuruga amani ya nchi, nina imani kabisa na hili maana hata vikundi kama al-shabaab, al-quaeda, isis, boko haram na vikundi vingine vilianza kama hivi hivi.!! Nawajua vizuri viongozi hawa sio kwamba wana uchungu zaidi na nchi kuliko wengine ila waroho tu wa madaraka na wanatumiwa na nchi au vikundi vingine nje ya Tanzania kuivuruga amani ya nchi. kwani lazima kuwe na vurugu katika kudai haki yenu? mbona Tanzania ilipigania uhuru na kuupata bila kumwaga damu za watu wasio na hatia?
Post a Comment