Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi na Balozi wa kampeni ya "Fun For Funds",
Madaraka Nyerere (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam dhumuni lake la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili
ya kuchangisha fedha za jukwaa la sanaa na ubunifu ili kukuza vipaji
vya vijana kupitia mafunzo mbalimbali ya sanaa na kutoa muongozo wa
jinsi ya kuanzisha wazo la ubunifu na kulikamilisha.Na
kuongeza pia vijana wataunganishwa na majukwaa mengine kama hili kwa
nchi za Afrika Mashariki kama vile The Nest, PAWA 254 na Creative Garage
yote ya Kenya na Africa Sanaa Kollective ya Uganda.
Balozi
wa kampeni ya kuchangisha fedha, “FUN FOR FUNDS” mwanamuziki mzalendo
mzee wa ‘Sumu ya Teja’ , Vitali Maembe akizungumza na waandishi wa
habari ambapo amewataka wasanii wenzake kuungana kuwa kitu kimoja katika
kukuza utamaduni wetu kwa kubadilishana uzoefu wa kazi zao bila choyo.
Mjumbe
wa bodi ya shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East
Africa (CDEA), Rose Haji Mwalimu akitoa rai kwa waandishi wa habari
waliohudhuria mkutano huo (hawapo pichani) na kuwataka kutumia kalamu
zao vizuri na kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa.
Madaraka
Nyerere, Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, pamoja na
Mwanamuziki Mzalendo Vitali Maembe wameteuliwa na shirika lisilo la
kiserikali Culture and Development East Africa (CDEA) kuwa mabalozi wa
kushiriki kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha jamii
kuchangia ujenzi wa jukwaa la sanaa na ubunifu jijini Dar es Salaam.
Kampeni
hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro imeandaliwa na CDEA kupitia njia ya
kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 7 hadi 13 mwaka huu ili
kujenga jukwaa na sanaa na ubunifu litakalowapa fursa wasanii na vijana
kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja ambapo mawazo ya kisayansi
yatakutana na sanaa na pia sanaa kukutana na taaluma nyinginezo nyingi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa anasema “ili kufanikisha kampeni yetu
ya mwaka mmoja tuliyoipa jina la ‘FUN FOR FUNDS’, tumeona ni vyema
kupanda mlima Kilimanjaro kwa kumtumia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi
ya CDEA, Madaraka Nyerere pamoja na Vitalis Maembe ambaye ni
mwanamuziki mzalendo”
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development
East Africa (CDEA), Ayeta Wangusa (wa pili kushoto) akielezea lengo la
kuanzishwa kwa Jukwaa la sanaa na ubunifu ambalo vijana watapata fursa
ya kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja.
Wangusa
anasema fedha zitakazopatikana kwenye kampeni hii maalumu zitatumika
kusaidia uzalishaji wa kazi za ubunifu za njia mbalimbali za
mawasiliano-bunifu, kuwekeza katika kuanzisha maabara ya Filamu(yaani
film lab) na kuchangia gharama za uendeshaji wa shughuli za Jukwaa la
sanaa na ubunifu.
Kwa
upande wake Madaraka Nyerere anasema, “Nimekuwa nikipanda Mlima
Kilimanjaro mara kwa mara kwa lengo la kuchangia ujenzi wa shule na
shughuli nyinginezo za maendeleo, hivyo mwaka huu nimeona nifanye jambo
hili kuhamasisha uchangiaji wa jukwaa hili la sanaa na ubunifu kwa
kushirikiana na CDEA”.
Madaraka
anawaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia katika kampeni hii ili
kufanikisha kufikiwa kwa lengo lake. “Wadau watakaopenda kuunga mkono
zoezi hili,wanaweza kutuma michango yao kwa njia zifuatazo: M-PESA:
0765544714, TIGOPESA: 0713160668 Au Benki: CRDB BANK PLC, Jina la
Akaunti: CULTURE AND DEVELOPMENT EAST AFRICA TZS ACC: 0150210421400, USD
ACC: 0252210421400, SWIFTCODE: CORUTZTZ”
Kwa
upande wake Mzee wa ‘Sumu ya Teja’, Vitali Maembe amesema pamoja na
kuwa hii ni mara ya kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro amefanya mazoezi ya
kutosha kumuwezesha kufika kwenye kilele jambo ambalo ni ndoto yake
kubwa kama mwanamapinduzi wa kimuziki.
Culture
and Development East Africa (CDEA) ni shirika lisilo la kiserikali
linalotoa huduma kwa wasanii, viongozi wa utamaduni, wajasiriamali,
maafisa utamaduni na mipango miji. Pia hufanya kazi na Mashirika makubwa
ya kimaendeleo, taasisi za kiraia na Elimu katika maendeleo ya
utamaduni, mipango na utekelezaji kwa Tanzania na Ukanda wa Afrika
Mashariki kwa ujumla.
Vitali Maembe akitoa vionjo vya wimbo wake Vuma.
Vitali Maembe akionyesha moja ya kazi zake za sanaa atakazoenda kuzitundika kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro panapo majaliwa.
Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Afisa
Habari wa shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East
Africa (CDEA), Mandolin Kahindi akitambulisha viongozi wa CDEA kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) pamoja na dhumuni la kuitisha
mkutano huo.
No comments:
Post a Comment