Saturday, September 27, 2014

MAADHIMISHO YA MAGEREZA DAY NCHINI ZAMBIA YAFANA

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania watatu kutoka kulia Akiwa katika Picha ya pamoja Mara baada ya chakula cha Jioni kilichoandaliwa kwa heshima ya kutambua na kuthamini mchango wa Rais na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika na masuala ya Wafungwa inayojulikana kwa jina la Prisons Fellowship International bwana Gordon Loux wa pili kutoka kulia.Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Radisson Blu Mjini Lusaka tarehe 25 Septemba,2014 siku moja Kabla ya Maadhimisho ya Magereza Day ili kutambua Mchango wa Taasisi hiyo kwa Magereza Zambia.Wanne kutoka kulia ni Bi Maureen Mwanawasa mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Mh.Levy Mwanawasa.Wa pili Kutoka kushoto katika Picha ni Kamishna Percy K Chato Mkuu wa Magereza Nchini Zambia na watatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali Raphael Tuhafeni Hamunyela Mkuu wa Magereza Nchini Namibia.Na wa kwanza kutoka kushoto ni Bi Ireen Chato Mke wa Kamishna Chato.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bwana John Casmir Minja,akisalimiana na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Africa Prisons /Correctional Service Day Zambia.Mheshimiwa Nickson Chilangwa (MP) wakati akiwasili Kwenye Viwanja Vya Chuo Cha Maafisa Magereza Mjini Kabwe Zambia Leo tarehe 26 Septemba,2014.
Kamishna Jenerali wa Magereza Bwana John Casmir Minja akiongozana na wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia wakielekea Kwenye jukwaa kuu Kabla ya kuanza kwa ratiba.
Kamishna Jenerali wa Magereza bwana John Casmir Minja akiwa na wakuu Wengine wa Vyombo vya ulinzi na usalama Nchini Zambia wakipokea salamu ya heshima kutoka kwa Maafisa na Askari Magereza hawapo pichani wakati wakipita Mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo wa pole na haraka.
Maafisa na Askari Magereza Nchini Zambia wakipita Mbele ya jukwaa kuu kwa mwendo haraka.
Baadhi ya Maafisa na Askari Magereza na wageni Wengine Waalikwa wakifutilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yanafanyika Leo Kwenye Viwanja vya Chuo cha Maafisa na Askari Kabwe wakati wa Maadhimisho ya siku ya Magereza Zambia.
Kamishna Jenerali wa Magereza mwenyekiti sare ya Kijani akiwa na Mgeni Rasmi pamoja na mwenyeji wao Kamishna Percy Chato Mkuu wa Magereza Nchini Zambia wakiaangalia kazi za aina tofauti tofauti zinazo fanywa na Maafisa na Askari pamoja na Wafungwa Kwenye mabandambalimbali katika Viwanja vya Chuo Cha Maafisa na Askari Kabwe.
Wakuu wa Magereza Nchini Tanzania na Burundi wakiwa katika Picha ya pamoja na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Magereza Day,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Nchini Zambia,Mh.Nickson Chilangwa (MP).Wengine walio kaa ni Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama Nchini Zambia.Pamoja na mambo mengine Mh. Naibu aliwatunuku Nishani mbalimbali baadhi ya Maafisa na Askari Magereaza kwa kutambua mchango wao katika ujenzi wa Taifa.Kuli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "Building a Sustainable and Humane Correctional System in Africa:A Collaborative Responsibility.Picha zote na mpiga Picha wa Makao Makuu ya Magereza Dar Es Saalam.

No comments: