Sunday, September 14, 2014

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE MIKOA YA PWANI,TANGA NA IRINGA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MKURANGA -PWANI) 2 
Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo. 3 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo. 5 
8 

Baadhi ya wakuu wa wilaya za mkoa wa Pwani kutoka Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi 16 
Mmoja wa viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Bi Agricola akiwa katika mkutano huo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutumia katika mkutano wa hadhara mjini Kimanzichana, wilayani Mkuranga, Pwani , alipoanza zira ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi
inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kinana aliwataka viongozi wa chama na serikali waliojilimbikizia vyeo na kushindwa kutekeleza wajibu wao, waanze kujiuzulu baadhi ya vyeo ili wapatiwe wengine wasio na vyeo kwa lengo la kukiendeleza chama na shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 01.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na chipukizi wakati wa mapokezi katika Kijiji cha Kipala Mpakani, wilayani Mkuranga, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezw
 02.Kinana akikagua gwaride la chipukizi  wakati wa mapokezi hayo.
 Nape (kulia) akiwaongoza wananchi kubeba matofali ya kujengea  jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Adam Malima  (kulia)akiwaongoza wananchi kubeba matofali ya kujengea jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana kuhutubia na kusikiliza kero za za wananchi katika Kijiji cha Kimanzichana.
 Kinana akisalimiana na wananchi
 Mwendesha bodaboda akiwa amelala baada ya kugongwa na gari wilayani Mkuranga katika Barabara Kuu ya kutoka Dar kwenda Mtwara. Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana ulisimama kwa muda katika eneo hilo na viongozi wa CCM akiwemo Kinana waliteremka kwenye magari na kusaidia kubeba majeruhi kuwaweka kwenye magari kuwawahisha kwenda hospitali kwa matibabu.

 Baadhi viongozi na wanachama wa CCM waliokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinanawakisadia kumbeba mwendesha bodaboda alijeruhiwa baada ya kugongwa na gari wilayani Mkuranga, wakimpeleka kwenye gari ili awahishwe kwenda hospitali kwa matibabu. Baada ya kufika kwenye tukio hilo Kinana alisimamisha msafara wake na kwenda kusaidia majeruhi wa ajali hiyo.
Gari lilihusika katika ajali na bodaboda likiwa kichakani baada ya kuacha njia
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kimanzichana.
Kinana akisaidia kujenga jengo la maabara katika Shule ya Sekondari ya Mwarusembe, wilayani Mkuranga

No comments: