Sunday, September 28, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA APOKELEWA KWA KISHINDO WILAYANI LUSHOTO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.
Umati wa wakazi wa kata ya Mlola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wananchi hao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai, kata ya Mlola ambapo aliwaambia wawe makini na matapeli wa ardhi wanaokuja kwa jina la Uwekezaji kwani wamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi nchini.
 Wazee Maarufu wa kijiji cha Lwandai wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara za kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pia katika mikutano yake ya sasa Katibu Mkuu amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi kuhoji maswali ,kutoa maoni au ushauri kuhusu maendeleo yao katika maeneo yao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilaya Lushoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamn Kinana  na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia mkono mamia ya watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilayani Lushoto.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lwandai ambapo aliwaambia wawe makini na maneno ya wanasiaa ambao wanahusisha hoja ya katiba mpya na uchaguzi wa mwaka 2015, alisema kuwa kuna watu wana sahau kuwa hiyo siyo ajenda ya wananchi na si makubaliano ya vyama vya siasa .
 Wananchi wa Mlola wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Kila kona ya uwanja ilijaza watu.
 Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali yanahusu maendeleo ya wilaya hiyo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ,Lushoto mkoani Tanga.
 Nyuso za matumaini za wakazi wa Mlola.
Deogratius Kisandu akiwasalimia wananchi wa Lwandai kata ya Mlola wilani Lushoto baada ya kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .Deogratius alishawahi kuwa na nyanzifa zifuatazo kwenye chama cha NCCR Mageuzi,Katibu Mwenezi Taifa  kitengo cha Vijana (2013) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya NCCR-Mageuzi (2014)
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiondoka eneo la mkutano huku akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga.
 Vitalu vya miti kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka mbole kwenye vitalu vya mradi wa upandaji miti Kwesimu muda mchache kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichambua mche wa mti wakati wa kuandaa vitalu kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu,Katibu Mkuu alisisitiza watu kujali na kutunza mazingira yao . 

No comments: