Mh.
Dr. Christine Ishengoma Mkuu wa Mkoa wa Iringa akipokea taarifa kuhusu
mfumo wa taarifa za masoko kutoka TAHA unavyofanya kazi zake kutoka kwa
Cyrila Antony Afisa wa Masoko
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Mh. Dr. Christine Ishengoma akisikiliza maelezo
kutoka kwa Mtaalamu wa kilimo wa TAHA Bw Ringo kuhusu uzalishaji wa zao
la nyanya
Elimu ikiendelea kutolewa.
Vitalu na green houses
Aina Mbalimbali za matunda ambazo zimezalishwa na wakulima kutokana na elimu Bora waliyo ipata kutoka TAHA
Mwananchi akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa TAHA
Teknolojia ya umwagiliaji kwa mfumo wa kilimo cha matone ambao pia unaonesha utengenezaji bora wa matuta, nafasi na usafi
Hivi ni Vitalu vya TAHA na Barton Tanzania
Vitalu vya mboga na green house kama zinavyoonekana katika picha
Watangazaji wa Radio Sweet FM ya Mbeya wakishangaa ubora wa karoti ambayo ni daraja la kwanza inapopelekwa sokoni
Zao la chines
Zao la karoti lililopandwa kwenye vitalu vilivyopo ndani ya viwanja vya Nanenane Mbeya kwenye Banda la TAHA
Mwananchi akifurahia maelezo kuhusu zao la karoti daraja la kwanza
********************
Wakulima
na wananchi mkoani Mbeya wameendelea kuneemeka na elimu ya bure ya
uzalishaji wa mazao ya mboga, viungo na matunda inayotolewa na Asasi ya
wakulima, wafanyabiashara na watoa huduma ya mazao ya horticulture
nchini Tanzania (TAHA).
Wakulima
hao wameneemeka na elimu hiyo inayotolewa na maafisa wa ufundi wa
kilimo kutoka TAHA kwa ushirikiano na wale wa Barton Tanzania ambao kwa
pamoja wameweka kambi katika viwanja hivyo ili kuhakikisha jamii ya
wakulima wa mboga kutoka ukanda wa Nyanda za Juu Kusini wanapata elimu
ya msingi bora ya uzalishaji wa mboga wenye tija.
"Mpaka
sasa tumetembelewa na wananchi na wakulima wasiopungua 460 ambao
wamefika katika banda letu hapa Nanenane kwenye viwanja vya John
Mwakangale wakitaka kujifunza mbinu na misingi ya awali ya uzalishaji wa
mazao ya horticulture, hiyo ni ishara njema kwani inaonesha ni kiasi
gani wananchi wanatafuta mbinu fasaha inayoweza kuwakwamua kutoka
katika uzalishaji wa mboga wa kawaida mpaka uzalishaji wa tija
unaozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa" Alisema Likati Thomas
afisa Mawasiliano kutoka TAHA.
Akifafanua
zaidi kuhusu elimu ya kilimo cha uzalishaji wa mboga kwenye banda la
TAHA afisa mawasiliano huyo alisema kuwa wamepanda mazao tofauti katika
ploti zilizopo kwenye eneo lao ambapo wakulima na wananchi wanaopata
fursa ya kutembelea eneo hilo ujifunza teknolojia mbalimbali za
uzalishaji kama vile uzalishaji unaozingatia Mbegu bora zenye tija.
Teknolojia
nyingine ni pamoja na upandaji mazao unaozingatia nafasi kati ya miche
na miche, umwagiliaji kwa njia ya matone(drip irrigation) unaozingatia
uhifadhi wa maji na mazingira pamoja na ulimaji wa matuta yaliyoinuka
ili kutoa nafasi kwa mizizi ya mimea kupenyeza kwenye udongo ili
kujitafutia lishe.
Mbali
na elimu hiyo ya uzalishaji wa mboga, wananchi wa Mbeya wanaotembelea
banda hilo pia wanapata fursa ya kujifunza elimulishe kutoka kwa
mtaalamu wa masuala ya lishe wa TAHA Bi. Lawrencia …..ambaye amekuwa
akiwafundisha wananchi juu ya umuhimu wa ulaji wa mboga na faida zake
kwa afya ya miili yetu.
No comments:
Post a Comment