Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi
(Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika
katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL. Wakishuhudia ni
baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya IPTL.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi
(Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika
katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL.
Mwenyekiti
Mtendaji wa kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited
(IPTL), iliyo chini ya Pan Africa Power Solutions (PAP), Bw. Harbinder Sethi
(Kushoto), akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) maboresho yaaliyofanyika
katika kiwanda hicho tangu PAP ilipochukua uongozi wa IPTL. Akishuhudia
ni Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni hiyo Bw. Parthiban Chandrasakaran.
Mahitaji makubwa ya umeme nchini yataweza
kupatiwa ufumbuzi kwa kuhakikisha kuna uzalishaji ziada wa umeme kwa kutumia
teknolojia zinazokubalika na nishati iliyopo Tanzania.
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa
kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kampuni
iliyo chini ya Pan African Power Solutions (PAP) wakati wa ziara ya wandishi wa
habari walipotembelea mitambo ya ufuaji umeme ya kampuni hiyo iliyopo Tegeta
jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Alisema kuwa IPTL inaamini kwamba usambazaji
wa umeme unaweza kuboreshwa kutoka megawati 800, ambazo kwa sasa zinahudumia
watu zaidi ya milioni 51.1 ambao mahitaji yao yanaweza kuzidi megawati
2000.
“PAP/IPTL inaamini kuwa soko bado ni kubwa na
si tu IPTL, bali pia na makampuni mengine yanapaswa yachangie katika kukuza
uwezo wa gridi na uzalishaji wake ili kufikia matakwa ya watanzania wapatao watu
milioni 51.1 kama ilivyokadiriwa katika sensa iliyofanyika mwaka 2014,” alisema
Bw. Sethi.
Alibainisha kuwa kupitia usambazaji wa umeme
wa uhakika na sera nzuri ya uwekezaji, Tanzania itapiga hatua ya kimaendeleo kwa
kasi na kuwa moja kati ya nchi kubwa kiuchumi Afrika katika siku za
karibuni.
“Kama wawekezaji watahakikishiwa umeme wenye
gharama nafuu na sera nzuri ya uwekezaji inayolinda pande zote mbili, viwanda
vingi vitajengwa nchini kwasababu Tanzania imebarikiwa kuwa na wingi wa mali
ghafi. Viwanda na miundombinu mizuri ni moja kati ya vigezo ambavyo wachumi
utumia katika kutambua maendeleo ya nchi,” alisema.
Alisema kuwa kuna ushaidi tosha unaoonyesha
jitihada za kuhakikisha kuwa nchi inaondokana na umaskini, baada ya
kuorodheshwa miongoni mwa nchi za kiafrika ambazo uongezekaji wa watu wake
umebaki thabiti na kukuwa kwa kasi kwa maendeleo ya watu walio na uchumi wa kati.
Ongezeko la uwekezaji katika miundombinu
unaongeza mahitaji ya umeme na usambazaji ambao pia unasaidia kukuza viwango
vya pato la taifa (GDP).
Bosi huyo wa IPTL/PAP alisema kuwa kampuni
yake ameeleza jitihada zake katika kuongeza uwezo wa umeme nchini kwa kuweka
mipango kazi ya utanuzi madhubuti na kupunguza viwango vya tozo katika bei ya
umeme kwa kuwajali wateja.
“Awamu ya kwanza ya mpango wetu umelenga
kuweka mtambo wa megawati 200 wa gesi ambao utakua karibu na mtambo wa sasa wa
megawati 103 wa IPTL unaotumia mafuta mazito (HFO). Mazungumzo juu ya hili bado
yanaendelea na mamlaka husika. Kama yote yatakwenda vizuri, mpango huu
utamalizika ifikapo mwezi Aprili 2015.
“Ikiwa kama ni sehemu ya awamu ya kwanza,
tutaweka kituo kidogo kipya chenye 220kv ambao ni muhimu sana kwa Tanesco kwa
ajili ya usambazaji katika kanda zote mpya mbali mbali za maendeleo huko
Bagamoyo na Chalinze. Hii ni pamoja na laini ya 220kv ya Ubungo,” alisema.
Bw. Sethi alibainisha kuwa awamu ya pili –
itakuwa ni uwekaji wa mtambo wa megawati 300 wa gesi pembezoni mwa mtambo wa
IPTL.
Alisema kuwa mtambo wa sasa wa IPTL utaendelea
kuendeshwa kwa kutumia mafuta mazito (HFO) endapo kutakuwa na tatizo katika
gridi ya taifa hususani la gesi asilia au matumizi ya mafuta.
No comments:
Post a Comment