Kina mama wakionyesha mfano wa kuwanyonyesha watoto wachanga katika
kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika
kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya
Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani
Iringa.
mwakilishi wa
shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania Paul Edwards akizungumza. (picha zote na Denis Mlowe)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Charles Pallangyo akizundua kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya
Ulishaji wa watoto wachanga na wadogo katika kilele cha maadhimisho ya
wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi
mkoani Iringa Juzi (kushoto) ni kaimu mkurugenzi wa mtendaji wa taasisi
ya chakula na lishe tanzania Dk. Joyceline Kaganda na katibu tawala mkoa
wa Iringa Wamoja Ayubu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo
akionyesha kitabu maalum cha Mwongozo wa Mafunzo ya Ulishaji wa watoto
wachanga na wadogo mara baada ya kukizundua rasmi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji
Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi
(kushoto)ni katabu tawala mkoa wa Iringa na kulia nimwakilishi wa Unisef tanzania Paul Edwards.
Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiigiza
kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa.
Wanajeshi wa KJ Mafinga wakiimba kwa hisia kali kuhusu janga la Ukimwi katika wiki ya
Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani
Iringa.
Baadhi ya wanafunzi wa uuguzi wakiwa katika maandamano wiki ya
Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani
Iringa.
Msanii
wa marufu nchi Emanuel Mgaya 'Masanja' akiongoza maandamano ya
kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji
Duniani yaliyofanyika kitaifa wilayani Mufundi mkoani Iringa Juzi.
Na Denis Mlowe,Mufindi.
SERIKALI imewataka waajiri katika taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kuzingatia na kulinda sheria zinazowalinda wanawake wanaojifungua kwa kuwapa likizo za uzazi kwa kuzingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 6 ya mwaka 2004 pamoja na kanuni zake.
Akizungumza katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya Unyonyeshaji Duniani yaliyofanyika kitaifa wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa juzi, mgeni rasmi Katibu wa Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii, Charles Pallangyo, mwanamke aliyejifungua mtoto mmoja anatakiwa
kupewa likizo ya uzazi ya siku 84 na aliyejifungua watoto mapacha anapewa
likizo ya siku 100.
Alisema likizo hizo zinaambata na
malipo kamili ya mshahara na mama aliyejifungua anaweza kuchukua likizo yake ya
mwaka akihitaji na mzazi aliyerudi kazini baada ya likizo ya uzazi anapewa
ruhusa ya saa mbili kwa siku kwenda kumnyonyesha mtoto.
Pallangyo aliwaasa wadau wengine
wanaojishughulisha na uuzaji wa maziwa mbadala ya watoto, mikoa na halmashauri
zote kujua na kufuata kanuni za kitaifa zilizotungwa chini ya sheria za mamlaka
ya chakula dawa na vipodozi sura ya 219 kudhibiti uuzaji na usambazaji wa
maziwa mbadala ya watoto pamoja na bidhaa zinazoambatana na vyakula vya watoto.
Aidha alivitaka vyombo vya habari
kuelimisha wanafamilia na wanawake hasa wanawake wanaojiita wa kileo ambao
wanaiga tamaduni za kigeni za ulishaji watoto ambazo mazingira yake ni potofu.
“Tungependa kuwaona hawa wanawake
wa kisasa wanabadilika na kuelewa kuhusu umuhimu wa kunyonyesha watoto hasa
katika miezi sita ya mwanzo ili kuwajengea watoto msingi mzuri kimwilina
kiakili hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo
kamati za lishe za mikoa na wilaya ili kuhakikisha kwamba elimu inatolewa kwa
wanawake wote” alisema Pallangyo
Awali Mkuu wa mkoa wa Iringa
Christine Ishengoma katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala mkoa wa
Iringa, Ayubu Warioba, aliitaka jamii kuelimishana kwenye kaya na jamii kuhusu
unyonyeshaji na ulishaji sahihi wa watoto katika ustawi na maendeleo ya jamii
na taifa kwa ujumla.
Alisema jukumu la kuboresha afya
na uhai watoto wa kitanzania ni la wananchi wote likianzia na mtu binafsi na
familia kwa ujumla.
Kwa upande wake mwakilishi wa
shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) nchini Tanzania Paul Edwards alisema shirika hilo na wadau
wengine linalenga kuimarisha unyonyeshaji
wa maziwa ya mama kama njia ya ufanisi na kuokoa maisha ya mtoto.
Alisema shirika hilo litawajengea
uwezo watoa huduma za afya kwenye vituo na wahudumu wa afya vijijini pamoja na
watu wengine ambao ni muhimu katika kufanikisha mipango ya kuboresha lishe kwa
watoto
No comments:
Post a Comment