Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo baada
ya kupata maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni kabla ya
kufanya ziara ya siku moja ya kutembelea Miradi iliyofadhiliwa na Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la
Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(wapili kulia) mchoro sanifu wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya waziri
mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar
es Salaam.
Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la
Kigamboni Mhandisi Karim Mattaka (kulia) akimuonyesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda
(wapili kulia) hatua za ujenzi wa daraja la Kigamboni, wakati wa ziara ya
waziri mkuu kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar
es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wapili kulia)
akitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni unaofadhiliwa na Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati wa ziara yake ya siku kutembelea miradi
mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Watano Kulia) katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa daraja la
Kigamboni ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi
mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba
wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu
Mizengo Pinda (wapili kushoto) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea
miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akitoa maelezo juu ya mradi wa NSSF wa nyumba
wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, kwa waziri mkuu
Mizengo Pinda (kulia kwake) wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea
miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto mbele) akitoa maelezo juu ya
mradi wa NSSF wa nyumba wa Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni
4,500, kwa waziri mkuu Mizengo Pinda (wapili kushoto mbele) wakati wa ziara
yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa inayofadhiliwa na NSSF
jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Meneja Miradi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (kushoto) akimuonyesha waziri mkuu Mizengo
Pinda (wapili kulia) moja ya sehemu za ndani ya mradi wa nyumba wa NSSF wa
Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500, unaondelea kujengwa,
wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayofsdhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (watano kushoto) katika picha
ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) mara baada ya kutembelea mradi wa nyumba za NSSF wa
Mtoni Kijichi wenye thamani ya shilingi bilioni 4,500 wa nyumba zenye gharama
nafuu, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku moja ya kutembelea miradi mitatu
mikubwa inayofadhiliwa na NSSF jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Dk. Ramadani Dau (kushoto) akitoa maelezo juu ya miradi ujenzi wa
kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village modern city Housing scheme' yenye
thamani ya matrilioni. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa na ziara ya siku moja
ya kutembelea miradi mikubwa ya miundombinu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata
maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake
alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village
modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za
kimarekani 544, 530, 562 unafadhiliwa na
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio
Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Wapili kulia) akipata
maelezo juu ya jinsi mabomba ya plastiki yanatengenezwa, wakati wa ziara yake
alipotembelea mradi wa Ujenzi wa kijiji cha kisasa unaoitwa 'Dege Eco Village
modern city Housing scheme' Jumamosi jioni. Mradi huo wenye thamani ya dola za
kimarekani 544, 530, 562 unafadhiliwa na
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 45 ya hisa na Azimio
Housing Estates Co. Ltd kwa asilimia 55 ya hisa.
Serikali imesema itajipanga ili kuona namna ya kukabiliana
na changamoto mbali mbali ambazo zitaweza kukwamisha miradi mikubwa
yanayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) yatakayo badilisha
sura ya Jiji la Dar es Salaam..
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda aliyasema hayo baadaa ya kutembelea miradi mitatu mikubwa
inayoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) amayo ni pamoja na
daraja la Kigamboni, mradi wa nyumba za gharama nafuu inayojengwa Mtoni Kijichi
na mradi wa nyumba Zaidi ya 7000 uitwao ‘Dege Eco Village iliyopo
Kigamboni.
Akizungumza
wakati wa kukamilisha ziara yake huko Dege Kigamboni katika mradi wa nyumba
Zaidi ya 7000 uitwao ‘Dege Eco Village’ Jumamosi , Pinda alisema
Kigamboni inendelea kwa kasi kubwa kiasi kwamba miundombinu iliyopo haitoshi
kuhimili idadi ya watu watakaohamia.
“Tunahitaji
kujipanga kwa dhati kuhakikisha barabara na vivuko vinafanya kazi.
Changamoto kubwa hapa ni barabara za viuongo kutoka Mandela upande wa Kurasini
na upande wa Kigamboni pia. Barabara hivi zote sita za darajani zitatakiwa
kufika Kigamboni, Mjimwema, Mbagala na kwingineko,” alisema.
Pinda
alisema daraja litakapo kamilika, watumiaji watatozawa tozo la barabara ili
kuweza kulihudumia. Alisema serilaki inafikiria pia namna ya kuipanga Kigamboni
ili iendane na maendeleo yanayokuja.
Kuhusu Mradi mkubwa wa Dege Eco Village
wenye uwezo wa kuchukua nyumba za gorofa Zaidi ya 7000 na za kawaida (villas)
300, Waziri mkuu alisema mradi huo utaleta msukumo mkubwa kwa maendeleo ya
taifa kwani hakuna mji utakao fanafana na ule kati ya miji mingi aliyofika.
Aliitaka
Manispaa ya Temeke kuangalia idadi ya watu kule Kigamboni ili serikali
iangalie uwezekano wa namna ya kupanga usimamizi kiutawala.
Pinda
alifurahishwa na kitendo cha NSSF kuwapa kipaumbele wanachama wake kupata
nyumba ambazo zimejengwa katika mradi wa Mfuko huo uliopo Mtoni Kijichi. Tayari
nyumba 85 zilizojengwa katika awamu ya kwanza zimeshachukuliwa na wanachama.
Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Novemba 2008 na kukamilika 2010.
Nyumba
215 zilizojengwa katika awamu ya pili nazo zimeshachukuliwa na wanachama na
baadhi ya wadau wengine. Nyumba hizo kwa mujibu wa Meneja Miradi, Mhandisi John
Msemo, zilianza kijengwa mwaka 2011 na kumalizika mwaka 2013 ikiwa ni awamu ya
tatu.
Mhandisi
Msemo alisema awamu ya tatu ndio inaendelea kwa sasa ya ujenzi wa gorofa na
nyumba za kawaida (villas) jumla yake ikiwa ni nyuma 820, mradi ambao ulianza
mwaka jana 2013 na unatarajiwa kumalizika 2015. Tayari nyumba 300 zimeshalipiwa
kabla hazijamalizika.
Akiongea
na waandhishi wa habari baada ya ziara ya waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
DK Ramadhani Dau alisema miradi yao ilikuwa inapata changamoto kubwa hasa
upande wa barabara.
“Tukimaliza
ujenzi wa daraja tunategemea barabara zote jijini ziwe zimeisha ili kupunguza
msongamano katika daraja. Itakuwa haina maana kumaliza daraja wakati maungio
hayajakamilika,” alisema.
Aliongeza
pia kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza wa miradi hiyo
ikiwemo ya kutopata ardhi toka kwa wananchi kwa muda unaofaa, serikali
kuchelewa kutoa asilimia 40 ya sehemu yake katika mradi na pia masuala ya
kitaalamu katika ujenzi wa daraja.
Kuhusu
mradi wa nyuma Mtoni Kijichi, alisema walikuwa wanahitaji sana daraja
litakounganisha Mtoni Kijichi na Mbagala kwani nirahisi sana kuvuka sehemu hiyo
na kuingia kigamboni kiurahisi kuliko kutumia Zaidi ya kilometa 20 kuzunguka
katika daraja ili mtu afike Kigamboni au Mbagala.
Tatizo
la maji alisema walilazimika kuchimba visima wakati DAWASA waki jiandaa
kufanya taratibu za kuweka maji.
No comments:
Post a Comment