Meya wa jiji la Mwanza ya Mhe.Stanslaus Mabula akinyanyua juu albam za
mwimbaji Rose Muhando wakati alipozindua albam hiyo mkoani Mwanza leo
kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Albam hiyo imezinduliwa na Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula
ambaye alimwakilisha Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari
Makamba. Akizungumza katika uzinduzi huo wakati akitoa ujumbe
aliouwakilisha katika uzinduzi huo kutoka kwa Mh. Januari Makamba,Mabula
ameuelezea ujumbe huo kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo
kushawishi makampuni ili yadhamini pia matamasha ya muziki wa injili ka
ambavyo yamekuwa yakifuturisha vikundi na waumini mbalimbali wakati wa
mfungo wa ramadhan.
''
kwakuwa muziki wa injili pia unaeneza amani na upendo kwa jamii ya
watanzania, Hii itasaidia kupunguza gharama za uandaaji, jambo ambalo
kwa namna moja au nyingine litakuwa linarahisisha uandaaji wa matamasha
hayo ambayo yamekuwa ni chachu ya watu kuachana na maovu na kuwa watu
wema katika jamii'',alisema Mabula.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba pamoja na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama kulia na mwimbaji wa muziki
wa injili Bonny Mwaiteje katikati na Mwimbaji Chengula kushoto wakati wa
tamasha la uzinduzi wa Albam ya Shikilia Pindo la Yesu uliofanyika
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza mwishoni mwa wiki
akisindikizwa na waimbaji malimbali wa muziki huo akiwemo Ephraimu
Sekereti kutoka nchini Zambia.
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula akiteta jambo na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion wa Msama Alex, kulia anayefurahia ni
mwimbaji Rose Muhando.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akigawa albam ya Rose Muhando kwa Mh. Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula na Maaskofu waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza machache katika uzinduzi huo.
Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula kulia akiwa amesimama na
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion wakati wa uzinduzi huo kutoa
kulia ni waimbaji Chengula Bony Mwaiteje , Tumaini Njole na Rose
Muhando.
Mmoja wa waratibu wa uzinduzi huo Bw. Hudson Kampga akizunguza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Alex Msama.
Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba wakati wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Rose Muhando akikamua na wacheza shoo wake wakati
wa tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
Mwimbaji
wa muziki wa injili Rose Muhando akipagawisha mashabiki wake wakati wa
tamasha hilo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo
Umati wa maelfu ya wa waliohudhuria katika uzinduzi hu wakinyanyua mikono juu juu.
Mwimbaji Bony Mwaiteje akifanya vitu vya sarakasi jukwaani.
Miwmbaji wa kimataifa kutoka zambia Ephraim Sekereti ni mmoja wa waimbaji waliokonga nyoyo za mashabiki wa muziki wa injili.
Noa Vicoria Singers wakafanya vitu vyao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bwa. Alex Msama akifanya vitu vyake na MC Mwakipesile.
Miwmbaji Tumaini Njole akafanya mambo yake pia katika uzinduzi huo
Ni Full Burudani ya muziki wa injili.
Miwmbaji Tumaini Njole akiimba kwa hisia kali katika uzinduzi huo
1 comment:
nooma kweli..
Post a Comment