Monday, August 11, 2014

DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKAGUA BARABARA YA MWENGE-TEGETA, MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) PAMOJA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA ZA JUU TAZARA FLYOVER NA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa na Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada kulia wakipita juu ya Daraja la Lugalo mara baada ya kulikagua katika ziara ya Ukaguzi wa Barabara ya Mwenge Tegeta jijini Dar es salaam leo.
 Balozi wa Japan nchini Ndugu Masaki Okada akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadick wakipanda ngazi za daraja la juu la watembea kwa miguu flyover Ubungo katika ukaguzi wa Barabara za kupunguza Msongamano (BRT) Ubungo jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar Es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakwanza kulia akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakikagua moja ya madaraja makubwa katika barabara ya Mwenge-Tegeta jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kukagua daraja katika barabara ya Mwenge - Tegeta ambayo ujenzi wake umeshakamilika.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale aliyenyoosha mkono akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwenge-Tegeta ambao umekamilika.
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akizungumza na Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada wakati wa Ukaguzi wa Barabara za Kupunguza msongamano katika eneo la manzese jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadick , Balozi wa Japan Masaki Okada pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakisikiliza kwa makini maendeleo ya mradi huo.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akipita juu ya daraja la waenda kwa miguu katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam

No comments: