Wednesday, August 20, 2014

BARUA YA WAZI KWA GAZETI LA MWANANCHI NA BWANA HUMPHREY POLEPOLE KUHUSU URAHIA PACHA KWA WATANZANIA.

Naomba unipe nafasi nitoe maoni yangu kuhusu Urahi pacha nikijbu maoni yaliyoandikwa kwenye gazeti la mwananchi na bwana Humphrey Polepole. Maoni yake yamenishangaza sana na mtu huyu anaonekana ana hujuzi kidogo katika mambo ya uandishi na ameamua kutumua ujuzi wake kudanganya watu kuhusu swala hili la urahia pacha kwa watanzania.
Napenda iheleweke kwamba urahia pacha sio kitu kigeni Tanzania. Kimsingi na kimazingira tanzania inaruhusu urahia pacha. 1.kwa watanzania wote walio na wazazi wenye urahia tofahuti mpaka watakapofikisha miaka ishrini na moja. 2.Kwa wanzanzibar wanye urahia wa zanzibar na urahia wa Tanzania.
Tatizo lililopo sasa ni watanzania wanataka wanufaike na urahia wa nchi nyingine pia na sio watu wengine wanufaike na urahia wa Tanzania. Hofu inayowekwa na wasiopenda maendeleo ya watanzania ni kudanganya kuwa wakongo, wamarekan, wasomali  na wengineo ndio watanufaika na urahia pacha. Kitu ambacho sio kweli mkongo atakapotaka kuwa rahia wa tanzania lazima aombe kupitia uhamihaji ya tanzania urahi huo. Na kira nchi inasheria zake kuhusu uraia  wa kuomba, nchi kama tanzania inabidi huwe umekaa ndani ya nchi kwa miaka isiyopungua kumi.na bado uchunguzi utafanywa kuhusu tabia zako na huko ulikokuwa kabla ya kupewa urahia wa Tanzania. Kwani hata ukikamilisha taratibu zote hizo bado idara ya uhamiaji inaweza kukukatila kuwa rahia wa Tanzania . Sasa ofu ya kusema wageni wengi watanufaika na  urahia wa tanzania. Inatoka wapi.
KINACHOOMBWA NA WATANZANIA WENGI NI KUWA NA HAKI YA KUPATA URAHIA WA NCHI NYINGINE BILA KUPOTEZA URAHI WAKO WA TANZANIA. HUWE NA URAHI PACHA. HII LITAKAPORUHUSIWA WATAKAONUFAIKA NI WATANZANIA NA SIO WAGEN. WATANZANIA TUNATAKA URAHI PACHA, HATUOMBI SERIKALI IVUNJE MASHARIT YA KUPATA URAHI WA TANZANIA KWA WATU WASIO WATANZANIA.
Sasa naomba nijibu hoja za bwana Humphrey Polepole.
1.Mr. Humphrey Polepole anasema kwamba ”Tuchukue mfano mwingine, sasa tuna sera ya kuhudumu katika jeshi kisheria kwa vijana wetu kama sehemu ya kujenga ushupavu na kuimarisha uzalendo wao, tukiwa na uraia pacha tujiandae kuwa na Warundi, Wakongo, Wamarekani, Wakenya na Wasomali JKT tukiwafundisha uaminifu, utii na namna ya kuipenda Tanzania kwa moyo wote hata na ikibidi mpaka tone la mwisho la damu yao.”
Hoja hii aina msingi wowote, kama kwa sheria za sasa za Tanzania zinaruhusu kijana aliyezaliwa na wazazi wenye urahia tofahuti kuwa na urahia wa nchi zote mbili hadi atakapofikishe miaka 21. Hii inamaana kwamba atakuwa ameshamaliza JKT akiwa na urahia wa nchi mbili tofahuti. Na kama akiamua kuacha utanzania na kuchukua urahia wa mzazi asieyekuwa mtanzania bado atakuwa alishapitia mafunzo ya JKT na kumaliza. Sasa hilo la JKT halina maana yeyeyote.
2.Bwana huyu aneendelea kwa kusema   ”Zaidi ya yote, uraia pacha unavunja msingi wa haki ya usawa kwa sababu katika taifa moja, raia wanawekwa katika mafungu, wale wenye uraia wa zaidi ya nchi moja, ambao wanakuwa na haki zote nchini na haki zaidi kwingineko dhidi ya wale wenye uraia mmoja, ambao wana haki zote za hapa nchini pekee, lakini wote wako sawa nchini”
Hapa anajifunua zaidi kuonyesha kuwa yeye ana wivu binafsi kwa wale wanaoweza kupata urahia pacha kwa kuwa watunufaika huko kwingine. Kwasababu urahia pacha hautampa mtu haki ya kufunja sheria za nchi au kupewa uwaziri au ubalozi na kumnyima yule mwenye urahia mmoja. Kwani tumeona watu wa nchi mbalimbali waliovunja sheria tanzania wakishikwa na kufunguliwa mashitaka na kufungwa tanzania bila ya kuwa na urahia wa tanzania, kwa makosa waliyofanya Tanzania. Hivyo uwe na urahia pacha au usiwenao, wote tutafuhata sheria moja ndani ya tanzania. Na tutakuwa na haki sawa na hakuna atakayetuweka kwenye makundi labda huyu bwana mwandishi mr. Polepole
3.Bwana Polepole anasema ” Mapendekezo haya yalizingatia kuwa nchi itakapotambua uraia wa nchi mbili, haitakuwa na msingi wa kikatiba na kisheria wa kuwazuia raia wa nchi nyingine kubaki na uraia wao wanapokuwa raia wa kuandikishwa wa Tanzania kwa kuzingatia kuwa Jamhuri ya Muungano inapakana na nchi nane na italeta changamoto ya usalama na ulinzi.”
Rahia wa nchi nyingine anapojiandisha kuwa rahia wa Tanzania anakuwa rahia wa tanzania wa kuandikishwa, Huyu ni Rahia wa nchi nyingine sio mtanzania. Hapa sisi tunazungumzia Mtanzania kupata urahia wa nchi nyingine, nazani hajaelewa somo. Ina maana kuwa wewe ni mtanzania lakini huwe na haki kubaki na urahia wa tanzania na kuweza kupata urahia wa nchi nyingine. Kama ni swala la usalama hizo nchi zitakazompa mtanzania urahi wao ndio zinatakiwa ziwe na wasiwasi kwamba anaweza kufanya upelelezi kwa niaba ya Tanzania na sio vinginevyo. Kama tunampa mkongo urahia wa tanzania tunakuwa na wasiwasi anaweza kupeleleza kwa ajili ya kongo sasa mtanzania marekani atapeleleza kwaajili ya tanzania huko aliko na sio vinginevyo.
Unajuha swala hili hawa wenye wivu binafsi wanataka kuwatisha watu wengine kwa faida zao wenyewe. Wanaposema maslahi binafsi dhidi ya maslai ya nchi wana maana gani. Kwani hao binafsi ni kina nani na nchi ni kina nani. Tatizo lililopo ni kuwa wapo watu wengi waliozoea rushwa na njia za ujanja ujanja kupata riziki wanaojuha kuwa hawa wanaotaka urahia pacha wengi wao ni watu waliosoma nje na hawatohi rushwa na watakapopewa urahia pacha watarudi nyumbani kufanya kazi kwa moyo wote hivyo kuchukua nafasi za wezi na wala rushwa ndio maana mnaona vita inakuwa kubwa kwa swala hili la urahia pacha. Hakuna hasara yeyeyote atakayopata mwananchi wa kawaida au nchi kwa kuruhusu urahia pacha ni faida tu kwa walio nao na rahia wema wote.
Mimi sizani kama Bwana Humphrey Polepole anajuha siri za serikali au jinsi ya kulinda usalama wa nchi hii kuliko Rais Jakaya Kikwete, au Waziri Benard Membe. Waliosema waziwazi kwamba urahia pacha utaleta faida kwa tanzania na kuhinua uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.Sizani kama rais wetu angkubali hilo kama anaona litahatarisha usalama wa nchi hii kwa namna yeyeyote hile.
Unajua watanzania wengi walio nje ya nchi wana uwezo wa kati. Biashara watakazokuja kufanya tanzania bila hofu ya kuzulumiwa watakapokuwa na utanzania wao zitawanufahisha watu wa hali ya chini. Kwa mfano, Mtu atakuja kujenga nyumba,i wakati anajenga, atanunua vifaa vya ujenzi hapo nyumbani na atatumia mafundi ujenzi ambao ni wananchi wa kipato cha chini kujenga nyumba hiyo. Hao atawalipa na wao watapata pesa za kusomesha watoto wao. Watakaopata hasara ni hawa wakina Humphrey Polepole, wanawatumia hawa mafundi na hawataki kuwalipa pesa zao kwasababu mafundi hawatakwenda kwao tena.

Kwa kifupi hawa wanaopinga urahia pacha ndio wanamasilahi binafsi, na hawataki wananchi wanufaike na faida za urahia pacha. Wananchi hamkeni na ungeni mkono urahia pacha kama anavyofanya rais wetu na wengine wengi walio na masilahi ya kweli kwa taifa na sio binafsi kama Mr polepole na waliomnunua atoe makala hii kwenye gazet lake la mwananchi. Kichwa ni chako kitumie kuhamua vizuri kwa faida ya Taifa lote. Mnufahishe Polepole au imefika wakati na sisi wote tunufahike.  

Ahasante.
NYAGA NYAGA
maonimusoma@gmail.com

5 comments:

Mbele said...

Kwa leo, sipendi kuongea kirefu, bali nitauliza suali moja tu. Mimi nanafundisha kwenye chuo kimoja hapa Marekani. Nimefundisha hapa tangu mwaka 1991, na sijawahi hata kuwazia kuomba uraia wa Marekani au nchi nyingine yoyote. Uraia wangu ni wa Tanzania.

Suali langu ni hili. Mtu anayeomba uraia wa Marekani, anatakiwa kula kiapo cha kuukana uraia wa nchi anakotoka, na anaapa kuwa hayatambua mamlaka ya rais wa nchi ile juu yake.

Kwa maana hiyo, m-Tanzania akitaka uraia wa Marekani, anawajibika kuukana uraia wa Tanzania, na kuapa kwamba hayatambui mamlaka ya rais wa Tanzania juu yake.

Kwa hivyo, rais wa Tanzania akitembelea Marekani, halafu tunaambiwa kuwa amekutana na wa-Tanzania, huwa najiuliza kama kweli wote wanaohudhuria ni wa-Tanzania, ambao wanamtambua rais kuwa ni rais wao, au kama kuna usanii unafanyika hapa.

Mimi naongelea uraia wa Marekani, siongelei nchi nyingine. Papo hapo, napenda kuongeza kuwa Marekani yenyewe haipendelei raia wake wachukue uraia wa nchi nyingine. Taarifa hizo ziko tele mtandaoni na kwenye tovuti husika za idara ya uhamiaji ya Marekani.

Ningependa wewe au yeyote mwingine, afafanue suala hili, na pia ningependa wa-Tanzania, hasa walioko nyumbani, kuanzia vijijini hadi mijini, waelewe maana halisi ya m-Tanzania kuomba au kupata uraia wa Marekani.

Ninavyoona, wale wanaopigania uraia pacha, na wengi wao wako hapa Marekani, hawaelezi suala hili la kiapo cha Marekani. Na hata viongozi wa serikali ya Tanzania ambao wanalipigia debe suala la uraia pacha, hawaongelei suala hili la Marekani. Kwa nini?

Anonymous said...

prof Mbele,
nadhani umetoa maoni ya ufinyu kwa kujitumia wewe kama kigezo. Suala la uraia pacha ni kwa yule anayependa..sasa wewe hukutaka, usijitumia kama kigezo.
Kuhusu jibu la swalo lako soma hii:
http://canada.usembassy.gov/consular_services/dual-citizenship.html

"However, dual nationals owe allegiance to both the United States and the foreign country. They are required to obey the laws of both countries. Either country has the right to enforce its laws, particularly if the person later travels there. Most U.S. citizens, including dual nationals, must use a U.S. passport to enter the United States."

kuna nchi tele zinaruhusu uraia pacha na wa ule wa marekani, Afrika na kwinigneko, kama Ghana, Iran, Ufaransa, Poland, namibia..
--soma hapa chini...
http://www.immihelp.com/citizenship/dual-citizenship-recognize-countries.html

kwa hiyo wewe unaweza kuamua kuchukua uraia hata wa Burunid, ni hiari yako, au ukabaki na tanzania..haimaniishi wewe ni mzalendo kuliko wengine.
Tunajua mwl alikuwa na jina 'Julius', lakini Mobutu alipukutisha majina yote ya Kigeni na kuchukua ya Kiafrika kuonyesha uzalendo..sasa tunajua ukweli ni kuwa Mwalimu alikuw a Mwafrika zaidi kwa vitendo na maisha yake kuliko Mobuto Sseseko...

hupo??



Anonymous said...

Zaidi ya kutoona hoja ya muandika mada, nimeona tu kwamba ana matatizo ya matumizi ya herufi h. anaweka isipotakiwa na haiweki itapotakiwa. shida sana.

Anonymous said...

Bwana mbele Said,
Naona na wewe bado hujaelewa somo. Kama nilivyosema huko nyuma kwamba kira nchi ina sheria zake kuhusu kumpatia mtu urahia wa kuandikisha. Hayo unayosema ni masharit ya kupata urahia wa marekani. Na sio tatizo la watanzania kupata haki ya kuwa na urahia pacha.Hatuwezi kuzungumzia kiapo cha marekani kuzuia WATANZANIA wasiwe na haki ya kunufaika na faida nyingi zinazotokana na urahi pacha. Marekani sio nchi pekee waliyo watanzania ziko nchi nyingi zenye sheria tofahuti kabisa na zinatoa faida kwa mtu mwenye urahia wao.

Kuhusu watanzania walio na urahia wa marekani au watakoataka kuchukua urahia wa marekani hilo litakuwa tatizo la hao watanzania na serikali ya marekani. Na sio tatizo la watanzania wote na serikali ya Tanzania. Kwa maana serikali ya Tanzania itakuwa imeruhusu kuchukua urahia mwingine, lakini haijamlazimisha mtu yeyeyote achukue urahia wa marekani. Yeye kama mtanzania atakapokanyaga aridhi ya Tanzania atafuhata sheria za tanzania kama mtanzania yeyeyote yule. Kama watanzania hatuwezi kubadilisha sheria ya marekani lkn tunaweza kubadirisha sheria ya tanzania kuwanufahisha WATANZANIA.na kwa maslahi ya watanzania.

Anonymous said...

Bwana Mbele, kama una muda naomba uperuzi wikipedia kuongeza knowledge kuhusu hili swala http://en.wikipedia.org/wiki/Citizenship_in_the_United_States Sina uhakika kama unaishi hapa kwa green card or kwa H-1 visa working permit, naomba uelewe citizenship, green card or working permit sio kwa kila mtu. Nina uhakika hata linapokuja suala la uraia pacha, sio wote watakaochukua huo uraia pindi ikihalalishwa. Watanzania tuelimishane kwamba kama kuna wanaomba dual citizenship kwa sababu mbali mbali kama kuwekeza nyumbani, wengine kurudi pindi watakapo stahafu, wengine just kuwa confortable kwa kutoomba visa kwenye nchi yao, social security na medicare uzeeni na mengineyo mengi. Again ni vizuri umeishi hapa kwa amani tangu 1991 na hujaona umuhimu wa kuwa raia. Naomba usitumie kigezo hicho kuhisi wewe ni mtanzania halisi kuliko wengine na badala yake utambue kwamba hutaki uraia wa nchi mbili kwa sababu wewe personally huoni umuhimu wake kwenye maisha yako ya kila siku hapa marekani. Napenda kuwakilisha... Swordfish