Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa
mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa
shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
Mchango
huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo
kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari
za Jimbo hilo.
Akikabidhi
msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka
wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa
za mitaani.
Diwani
wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya
sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
“Nataka
niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi
viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo,
haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu
wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.
Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
“Mimi
inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na
wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu
vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa
Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
Diwani
wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200
kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe,
Lazaro Nyalandu.
Katibu wa Mbunge Lazaro Nyalandu , Elia Digha, msaidizi wa Mbunge Ellen Mutalemwa wakimsikiliza Mwenyekiti Hanje Kinyeto.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Mtinko.
Mwenyekiti wa CCM Singida vijijini, Narumba Hanje akizungumza na wananchi wa Kata ya Mtinko wakati wa kukabidhi mabati 220.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Singida Vijijini, Narumba Hanje (kulia) akimkabidhi
mabati 220 yenye thamani ya shilingi milioni tano Afisa Mtandaji wa Kata
ya Mtinko Jimbo la Singida Kaskazini, Eliufoo Mkanga katika hafla fupi
iliyofanyika jana katika shule ya Sekondari ya Kata ya Mtinko , mabati
hayo yametolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa maabara na Mbunge wa
Jimbo hilo Mhe,Lazaro Nyalandu.
Hili ni jengo la maabara ya sekondari ya Kinyeto likiwa katika hatua ya lenta.
Kibao kikionesha shule ya sekondari Mtinko.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
No comments:
Post a Comment