Maafisa
wa Ubalozi, Bwana Amos Msanjila na Dada Caroline Chipeta,
Wakimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe.
Mizengo Pinda na Mkewe (Mama Tunu Pinda) walipowasili katika Ofisi za
Ubalozi wa Tanzania, London
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Mizengo Peter Pinda akipokewa,
kukaribishwa na kusalimiana na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi pamoja na
Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania waishio nchini Uingereza.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria Mkutano wao na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda, alikutana
na kuzungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza siku ya Jumamosi
tarehe 12 Julai 2014, mara baada ya ziara yake fupi ya kikazi nchini
humo.
Mkutano
huo na Watanzania ambao uliofanyika Ubalozini, Mheshimiwa Waziri Mkuu
alitoa taarifa mbalimbali za maendeleo nchini, hususan mchakato wa
Katiba mpya, sera ya Diaspora na maandalizi ya chaguzi mbalimbali
zinazokuja. Mkutano huo
ulimalizika kwa maswali na majibu na baadae wananchi kupiga picha na
Waziri Mkuu kama inavyoonekana kwenye picha hizi hapo chini.
Watanzania waliofika kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda katika mkutano huo.
Wawakilishi wa Jumuiya za Watanzania, wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, alipokutana na kuzungumza nao
Waziri Mkuu akijiandikisha kwenye Kitabu cha Wageni kwenye Ofisi za Ubalozi
Mama Tunu Pinda, Mke wa Mhe. Waziri Mkuu akijiandikisha kwenye Kitabu cha Wageni Ofisini hapo.
Pichani, Kaimu Balozi, Dada Caroline Chipeta (Mkuu wa Utawala), akiongea machache kumkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu
Mtanzania, Bwana Chris Lukosi, akichangia na kutoa maoni yake kwa Watanzania wenzie waishio Uingereza
Mke wa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, akiongea na Watanzania waliofika kwenye mkutano wao na Mhe. Waziri Mkuu.
Mhe. Waziri Mkuu na Mkewe wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi
Maafisa
wa Ubalozi, Wawakilishi wa Jumhuiya za Watanzania wakiwa kwenye picha
ya pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Peter Pinda na
Mkewe Mama Tunu Pinda
1 comment:
Haya bwana waziri aje pia kututembelea wakazi wa kijiji cha mkanyageni
Post a Comment