Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa
ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni
utekelezaji wa miradi ya dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada
ya Mvua kubwa. Mradi huo ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za
Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo
itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.Picha Zote Na Dj Sek Blog
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.
No comments:
Post a Comment