Katibu wa mbunge wa jimbo la Kalenga Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi msaada wa bati 100 kwa uongozi wa kijiji cha Usengerendeti kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya wauguzi wa Zanahati ya kijiji . |
Wananchi wakishiriki kushusha bati hizo |
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa akieleza kazi mbali mbali zilizofanywa na mbunge Godfrey Mgimwa toka alipochaguliwa |
Katibu wa mbunge Mgimwa Bw Martine Simangwa kushoto akikabidhi bati 80 kwa uongozi wa serikali ya kijiji cha Mahanzi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kijiji hicho kipya |
Wananchi wakimpongeza katibu wa Mgimwa kwa niaba ya mbunge wao Godfrey Mgimwa
.............................................................................................
Na Francis Godwin Blog.
Na Francis Godwin Blog.
MBUNGE
wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa ametoa msaada wa bati 180
zenye tahamani ya zaidi ya Tsh milioni 1 kwa kata ya Wasa kwa kama
sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake katika kata hiyo.
Akikabidhi
msaada huo kwa niaba ya mbunge Mgimwa katibu wake Martine Simangwa
alisema kuwa bati hizo ni sehemu ya jitihada za mbunge huyo
kuunga mkono harakati za wananchi katika kuibua miradi ya
kimaendeleo katika maeneo yao.
Hata
hivyo alisema kuwa bati hizo 100 ni kwa ajili ya kijiji cha
Usengerendeti ambao wapo katika ujenzi wa nyumba ya waganga katika
Zahanati ya kijiji na bati 80 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule
katika kijiji kipya cha Mahanzi .
Alisema
kuwa moja kati ya mambo ambayo mbunge Mgimwa ameyawekea kipaumbele
zaidi ni pamoja na elimu pamoja na afya na kuwa jitihada za
kuhakikisha mambo hayo yanashughulikiwa zinafanyika .
Pia
alisema katika kuhakikisha maendeleo ya jimbo hilo la Kalenga
yanaendelea kusonga mbele zaidi ni vema wananchi wa jimbo hilo
kuelekeza nguvu zao katika maendeleo na kuachana na baadhi ya watu
wanaopita katika jimbo hilo kwa ajili ya kuutaka ubunge mwaka 2015.
Kwani
kufanya hivyo ni kuendelea kurudisha nyuma maendeleo ya jimbo hilo
na kuwataka wanaofanya hivyo kwa sasa kusubiri muda ukifika ndipo
wananze kujipitisha na kuwa kimsingi katika nafasi ya ubunge hakuna
mbunge kivuli hivyo kitendo cha watu hao wanaojipitisha kufanya hivyo
kwa sasa ni kuvuruga kasi ya maendeleo ya jimbo hilo.
Akizungumzia
kuhusu suala la afya katika jimbo hilo alisema kuwa hali ya huduma
ya afya bado si mbaya sana japo kuna changamoto mbali mbali ambazo
zinapaswa kushughulikiwa ikiwemo ya dawa pamoja ,ukosefu wa nyumba za
watumishi wa afya na baadhi ya maeneo zahanati na vituo hivyo vya
afya kukosa umeme.
Awali
wananchi wa kata hiyo ya Wasa walimpongeza mbunge huyo kwa
kuonyesha uaminifu kwao na hata kuanza kutimiza ahadi zake kwa
wakati mfupi zaidi ukilinganisha na wabunge wengine waliopata
kuongoza jimbo hilo ambao hadi wameondoka madarakani baadhi ya
ahadi hawajatekeleza kwa wananchi.
Alisema
Yohana Sanga kuwa jimbo la Kalenga kwa muda mrefu limekuwa ni
jimbo linaloongoza kwa kubadili wabunge kwa kila kipindi kimoja na
ndi sababu ya jimbo hilo kuendelea kuwa nyuma katika maendeleo
ukilinganisha na majimbo ambayo wabunge wake wameongoza kwa zaidi ya
kipindi kimoja na kuwa kwa sasa wao hawana haja ya kubadili mbunge
mwingine zaidi ya Mgimwa .
No comments:
Post a Comment