Tuesday, July 8, 2014

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MJINI MOSHI (MUWSA) YAFANYA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI KATIKA SIKU 360

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA,Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo (hawapo pichani) wakati wa kutimiza siku 360 ofisini.
Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,MUWSA wakimsikiliza Mkurugenzi wa mamlaka hiyo(hayupo pichani)
Meneja Fedha wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi ,Grace Msiru akizungumzia mafanikio na changamoto katika siku 360 kwa idara yake ya fedha.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA.
Meneja Biashara wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi ,MUWSA ,John Ndetiko akizungumzia mafanikio na changamoto katika siku 360 kwa idara yake ya Biashara.
Meneja utawala na rasilimali watu wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi,Michael Konyaki akizungumzia mafanikio na changamoto katika siku 360 kwa idara yake.
Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,MUWSA wakisikiliza kwa makini taarifa ya Meneja utawala na rasilimali watu ,Michael Konyaki(Hayuko pichani)

Mwenyekiti wa TUICO tawi la MUWSA Masoud Barrie akizungumza juu ya mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo .
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na maji taka mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja akigawa fomu za Bima ya Afya kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.
Mkaguzi wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi ,Benson Maro akizungumza katika kikao cha wafanyakazi wa Mamlaka hiyo baada ya kumaliza mwaka.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Musa Shah akitoa neno la shukrani baada ya kikao cha tathmini kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

No comments: