Tuesday, July 22, 2014

MAFUNZO YA TABIA NCHI KWA WATAALAMU YAFUNGULIWA MKOANI MOROGORO

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kushoto) akifungua rasmi mafunzo  yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro. Aliyekaa upande wa kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion  Kasege.
 Mmoja wa wawezeshaji Profesa Pius Yanda kutoka Kituo cha Taaluma ya Mabadiliko ya Tabianchi kilichopo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo
 Baadhi  ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na wawezeshaji kwa nyakati tofauti tofauti
 Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira Mhandisi Gidion  Kasege  (kulia) na Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP Bw. Theodore Silinge kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa
 Afisa Mazingira Mkuu na Mratibu wa Mradi wa EMA-ISP kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw. Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
 Mtaalamu kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Nyaso Makwaya akisisitiza jambo wakati alipokuwa  akiwasilisha mada kuhusiana na mikakati ya Wizara katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gidion  Kasege  (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava  (aliyekaa kulia kwake) ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo  yanayowakutanisha wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yanayoendelea mjini Morogoro.
 Washiriki  wa mafunzo ya Mabadiliko ya Tabianchi  yanayoendelea mjini Morogoro wakiwa katika picha  ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (wa nne kutoka kushoto waliosimama mstari wa mbele) mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo

No comments: