Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakipongezana mapema kipindi cha pili baada ya kuifunga bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya Timu ya Ijuganyondo amabao ndio walikuwa wamewatangulia kwa bao 1-0 tangu kipindi cha kwanza.Wachezaji wa Timu ya Kagondo FC wakipongezana baada ya Kipa wa Ijunganondo Fc Yassin Issa kujifunga bao kwa Uzembe wa kudaka mpira na kumponyoka na kuingia langoni mwake na Mwamuzi wa pembeni kuliona na kudai bao na hatimaye Timu ya Kagondo kufanya itangulie kwa bao 2-1.
Uwanjani ilikuwa mshike mshike!!! Kagondo tangu kipndi cha pili walikuwa wanausongo wa kuwafunga wenzao Ijuganyondo!
Baadae katika kipindi cha pili mwishoni Timu ya Ijuganyondo ilifanya Mabadiliko na kufanikiwa kusawazisha baada ya Straika wao kukatiza mbele ya Mabeki wa Kagondo Fc na kusawazisha bao na kufanya bao kuwa 2-2 na mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa kutoshana nguvu kwa sare ya 2-2. Mikwaju ndio iliamua nani anakwenda hatua ya Nusu Fainali kati ya Kagondo Fc na Ijuganyondo Fc. Timu ya Ijuganyondo ilikosa penati mbili na timu ya Kagondo Fc kukosa mmoja ambapo timu ya Kagondo iliibuka na Ushindi kwa Mikwaju ya penati 4-3 na kujikatia tiketi ya kwenda Nusu fainali katika Michuano hii ya Ligi ya Kagasheki.
Mpaka sasa katika timu nane tayari timu 3 zimeishatinga hatua hiyo ya Nusu Fainali ambazo ni Mabingwa watetezi Bilele Fc, Miembeni Fc, Kagondo Fc. Kesho ni kati ya Rwamishenye vs Kitendaguro kutafuta timu ambayo itakamilisha timu nne za kucheza Nusu Fainali. Ambapo Mshindi wa Kesho anatarajiwa kucheza na mshindi wa leo Kagaondo Fc.
Kipa Yassin Issa wa Ijuganyondo akidaka kwa uzuri kona
Habari zifike na Nyumbani
Taswira jukwaa Kuu wakitazama soka
Wachezaji wa Timu ya Kagondo Fc wakimpongeza mchezaji wao aliyewapa ushindi wa kwenda hatua ya Nusu fainali Abdallatifu Khamis juu kwa juu.kila Mtu na Tabasamu lake....
Ilikuwa Shangwe leo, Huku mashabiki wa Ijuganyondo Fc wakibaki midomo wazi kuona Timu yao inaondolewa katika Michuano hii ambako walikuwa wanaipa Matumaini tangu kipindi cha kwanza kusonga hatua ya Nusu Fainali.
No comments:
Post a Comment