Na Mwandishi
Maalum, New York
Wakati ni jambo lisilopingika na linalokubalika na
waafrika wenyewe na washirika wa maendeleo
kwamba uchumi Afrika unakua vizuri. Hata hivyo ukuaji huo
unaelezwa bado haujaweza kupunguza au kuondoka changamoto mbalimbali za
kimaendeleo zinazolikabili bara hili na
watu wake.
Na kwa sababu
hiyo imeelezwa kwamba ili afrika iwe na maendeleo endelevu na jumuishi basi
inahitaji kuongeza kasi ya kuvutia uwekezaji na mitaji kutoka ndani ya Afrika yenyewe na
nje.
Hata hivyo suala
kubwa na ambalo limekuwa likiwafikirisha
waafrika wenyewe na wataalamu wa
masuala ya uchumi na maendeleo ni hili , je ni aina gani ya
uwekezaji na wenye tija ambao
Afrika inauhitaji.
Katika siku
nzima ya Alhamisi Baraza kuu la Umoja wa
Mataifa lilikuwa na majadiliano ya kina yaliyojikita katika eneo la Uwekezaji
na umuhimu wake kwa maendeleo ya bara la Afrika na watu wake ni vile vile
mchango wake katika mchakato mzima wa maendeleo endelevu baada
ya 2015.
Mkutano huo ulifunguliwa na katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,
ambaye katika hotuba yake, pamoja na kusifia namna Afrika ilivyopiga hatua
nzuri katika ukuaji wa Uchumi, akaeleza
kuwa kama kweli Afrika ilikuwa inataka
maendeleo yamfikie kile mtu basi ilikuwa
inahitaji kufanya mambo matatu.
Kwa mujibu
wa Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, mambo hayo
ni kujiwekea mazingira mazuri
yatakayovutiwa wawekezaji , aina sahihi ya
miradi/ uwekezaji inayotakiwa kuwekezwa
na udhibiti mzuri wa mapato yatokanayo
na uwekezaji huo ili hatimaye yaweze kuhimili maendeleo endelevu.
Katika Mkutano
huo na ambao washiriki mbalimbali walipata fursa ya kuchangia mawazo yao, Ban
Ki Moon pamoja na kuelezea maeneo hayo
matatu, alianisha pia mafanikio kadhaa
na changamoto kadhaa ambazo anasema
Afrika inaendelea kukabilina nao, akazitaja baadhi ya change moto hizo
kuwa ni uwekezaji duni katika
miundombinu, kilimo, ajira kwa vijana,
utaalam na teknolojia anuai na
tatizo kubwa la nishati ya uhakika na ambayo haiwafikii watu wengi.
Katibu Mkuu alisifu mikakati na mipango
mbalimbali ya kimaendeleo, kiuchumi na kijamii, ambayo ama Viongozi wa
Afrika tayari wameshaanza kutekeleza
au ilikuwa katika hatua mbalimbali za
utekelezaji.
Alipopata nafasi
ya kuchangia maoni ya Tanzania kuhusu
umuhimu wa uwekezaji na maendeleo kwa
Afrika, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi yeye alieleza kuwa
pamoja na kwamba Tanzania ilikuwa inakubaliana na umuhimu wa uwekezaji kwa
maendeleo, uwekezaji huo unahitaji ushirikiano wa pamoja, uwazi na utawala bora.
Akaeleza kwamba
kama ilivyoelezwa na wazungumzaji
wengine, sura ya Bara la Afrika imebadilika sana, Afrika ya sasa si ile
iliyokuwa ikidharauliwa na kuonekana kama ni bara lisilo na muelekeo wowote.
Akasema
anakubaliana pia kwamba uchumi wa afrika
unakua vizuri na kuwa ukuaji huo umechangiwa na mambo mengi baadhi yake
ni pamoja na sera na mipango mizuri ya kiuchumi, uwepo wa
mazingira ya amani na usalama katika maeneo mengi ya Afrika na ukuaji ya kada ya watu wenye kipato cha kati
pamoja na wimbi kubwa la vijana ambao
nao ni mtaji wa aina yake.
Balozi Manongi
pia akagusia umuhimu wa uwekezaji katika
miundombinu, afya, elimu na kilimo kuwa ni baadhi ya maeneo ambayo kama yakiwafanyiwa kazi vizuri yatasaidia
katika kuifanya Afrika isonge mbele.
Hata hivyo Muwakilishi huyo wa Tanzania akasema kasi ya ukuaji wa uchumi wa Afrika, pamoja na
ule wa nchi moja moja na jitihada kubwa na nzuri zinazofanywa na viongozi wakuu wa nchi na serikali pamoja wakishirikiana
na wananchi wenyewe, zinaweza
kukwamishwa au zinakwamishwa na baadhi ya na changamoto kadhaa zinazohitaji ufumbuzi wa pamoja.
Moja ya changamoto hizo na ambazo amesema ni tatizo kubwa la linalochangia kurudisha nyuma juhudi za nchi nyingi za Afrika kujiletea maendeleo yao ni tatizo la utoroshwaji wa fedha au biashara ya
fedha haramu zinazofichwa nje ya
Afrika na kusababisha ukwepaji
mkubwa wa kodi.
Akasema utoroshwanji huo wa fedha na ambazo hazilipiwi
kodi zinazinyima nchi zinazoendelea mapato ambayo yangetumia kujenga hospitali,
shule, barabara na miradi mingineo ya
maendeleo pamoja na utekelezaji wa
malengo ya maendeleo ya millenia.
Changamoto
nyingine alizosema zinarudisha nyuma maendeleo ya Afrika ni pamoja na uvunuaji holela wa maliasili,
biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na za kati na rushwa.
Balozi Manongi akasema ni kwa sababu hiyo na nyingine nyingi ndiyo
maana Tanzania imekuwa ikiunga mkono
malengo ya maendeleo endelevu
ambayo kwayo yatachangia siyo tu kuwahakikisha maendeleo jumuishi kila mtu lakini pia yatakayoweza
kukabiliana na changamoto alizozitaja.
Baadhi ya
wawakilishi kutoka mataifa yaliyoendelea
waliozungumza katika mkutano huo
walijipambanua zaidi kwa kuelezea ni kwa namna gani nchi zao zimekuwa zikichangia katika maendeleo ya Afrika kwa
kutoa misaada mbalimbali ya kimaendeleo
yakiwamo pia masuala ya teknolojia.
Muwakilishi wa
Marekani katika mkutano huyo naye pamoja na kuelezea ushirikiano uliopo kati ya Marekani na Bara la Afrika kwa maana ya
maendeleo ya kiuchumi, alitangaza katika
mkutano huo kwamba, Serikali ya Rais Obama ilikuwa inaadaa mkutano kati ya Marekani na Afrika. Mkutano huo utaojadili
ushirikiano wa kibiashara na unarajiwa
kufanyika mwanzoni mwa wezi Agosti mwaka huu.
No comments:
Post a Comment