Mkurugenzi
wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda
na Biashara, Consolata Ishebabi akizungumuza
na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata
mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji
kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa
FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo
ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bi. Joan
Kitembe kutoka Mkoa wa Arusha, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika
mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya
kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion
Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo
ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bi. Bahati
Bukubilo kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika
mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya
kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion
Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo
ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bw. Linus Mwangoya kutoka
Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa pili kimkoa katika mashindano ya kuandika
mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili
kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa
wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo
ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bw. Bakari Khamisi kutoka
Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa tatu kimkoa katika mashindano ya kuandika
mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili
kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa
wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore (wa
nane kulia kwa waliosimama) pamoja na Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara
ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi
(kushoto kwa Marion) wakiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali kutoka
mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji
biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha
ya FAIDIKA.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore akizungumuza na wajasiriamali kutoka
mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji
biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha
ya FAIDIKA. Kushoto ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na
za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi na kulia ni
Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe
Taasisi
ya kifedha ya FAIDIKA, inayoshughulika na utoaji mikopo hapa nchini,
imewawezesha wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam baada
ya kuwapa mafunzo ya njia bora ya ufanyaji biashara.
Wajasiriamali
hao ni miongoni mwa wale 300 waliopata mafunzo na baadae kuingizwa katika
mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara, kisha kuwapata washindi watatu
katika kila mkoa.
Akizungumuzia
mashindano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema washindi
watano katika kila mkoa walipatikana baada ya kuwasilisha maandiko ya
mchanganuo wa biashara ambazo zilionekana kukidhi vigezo vilivyowekwa na walimu
wa wajasiriamali hao.
“Leo
FAIDIKA inatimiza ahadi yake ya kuwapa wajasiriamali ambao michanganuo yao ya
biashara imeonekana kuwa bora zaidi. Katika kila mkoa, mshindi wa kwanza
amepata Tsh milioni 1.2, mshindi wa pili Tsh 800,000, watatu 500,000, wanne Tsh
300,000 na wa tano kupata 200,000.
“FAIDIKA
ilifanya mashindano haya baada ya mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 300 kutoka
katika mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya makundi matatu:
Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye ulemavu asilimia 32 na watu wa
kawaida mitaani asilimia 34," alisema.
Awali,
mgeni rasmi katika hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa washindi, iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo
na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi aliwataka
wafanyabiashara ndogo ndogo kurasimisha biashara zao ili kuepuka usumbufu
wanaopata wa kupoteza mali zao na mitaji ya biashara wakati wa oparesheni ya
safisha mji.
Bi.
Ishebabi alisema biashara zilizorasimishwa na kupewa leseni, hupangiwa
utaratibu mzuri wa kufanyia shughuli za biashara, hivyo kumfanya mjasiriamali
awe na nafasi ya kutumia biashara yake kukopa mikopo katika taasisi mbali mAbali
za kifedha.
“Wafanyabiashara
ndogo ndogo wakijisajili katika mfumo rasmi, inakuwa rahisi hata kwa taasisi zinazotoa
mikopo kuwaamini na kuwapa mikopo na kuweza kutanua mitaji yao. Bila kuwa
rasmi, ni vigumu kuaminika. Kwa biashara zilizorasimishwa, oparesheni ya
safisha mji haiwaathiri kwani watakuwa katika maeneo maalum waliopangiwa
kufanya shughuli zao,” alisema Bi. Ishebabi.
Alipongeza
uongozi wa FAIDIKA kwa kuja na utaratibu wa kuwafuatilia wajasiriamali ili
kuhakikisha kuwa wanazingatia biashara walizoombea hela na kuwaonyesha njia
bora ya kuboresha biashara zao, na kuzitaka taasisi zingine zinazotoa mikopo
kuiga mfano huo, mbali na kujali tu kama mkopaji anarejesha mkopo.
No comments:
Post a Comment