Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii imeanza kutoa futari katika vituo vinavyolea watoto waliopo katika mazingira magumu nchini.
Kupitia mpango huu Airtel imetoa msaada wa chakula kwa kituo cha Sharif Saidi Al-Bath kinacholea watoto yatima kilichopo Nyegezi Majengo Mapya Jijini Mwanza
Akiongea wakati wa kukabithi msaada huu , Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana Raphael Daudi alisema” Airtel Kwa kutambua changamoto nyingi zinazozikumba jamii tumeonelea ni vyema katika mfungo huu wa ramadhani kutenga muda wa kutembelea na kutoa msaada kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima nchini. Leo tumetembelea kituo hiki cha Sharif Saidi Al-Bathi na kuwapatia msaada wa chakula ambacho kitawasaidi hata baada ya mwezi wa ramadhani.
lengo letu ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla, husasani watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha tunarudisha faida tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia shughuli zetu za huduma kwa jamii kila mwaka.
Kwa upande wake Kiongozi wa Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath bwana Alhaji Hussein Mussa Alisema” Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu, tumefurahi sana na kuona kumbe watanzania wenzetu na mashirika mbalimbali wanaunga mkono jitihada zetu katika kuhakikisha tunawalea na kuwasomesha watoto yatima. Kituo chetu bado kina mahitaji mengi hivyo natoa wito kwa taasisi zingine kujiunga na kuendelea kusaidia kituo chetu na vituo vingine nchini
Baadhi ya watoto wanaoishi katika kituo hiki wameishukuru Kampuni ya Airtel kwa msaada wa vitu mbalimbali walivyotoa na kuyatala makampuni mengine kuiga yale yaliyofanywa na kampuni hiyo.
Vituo vingine vitakavyopata msaada kutoka Airtel ni pamoja na New Hope Family group-Temeke, Al-Hidaya children’s Home-ilala, Irishad Madrasah-Mbezi kwa Msuguri (kinondoni), Kiboa orphanage-Arusha na Heartfelt orphanage care Mbeya
Kituo cha Sharif Saidi Al-Bath chenye watoto Yatima zaidi ya 50 kilichopo Mwanza tayari kimepokea msaada kutoka Airtel mwishoni mwa wiki.
Meneja Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA) Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
|
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani..
|
Upakuaji ukiendelea.
|
Ni sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe, unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
|
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu (kushoto) akiwa na Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael wakisaidizana kufanikisha shughuli hiyo ya makabidhiano.
|
Mafuta kwa Kituo.
|
Vijana wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza katika picha ya makabidhiano na wadau wa Airtel.
|
"Hawa ni watoto wetu, hivyo tunapaswa kuwalinda" Kauli ya pamoja ya wadau wa Airtel kwa wale wote wenye mapenzi mema.
|
Twaha bin Bakari Utari ambaye ni Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA) ambao ni wamiliki na kituo ameshukuru kwa msaada huo toka Aitel huku akihamasisha wadau wengine kuiga mfano huo kwa ustawi wa jamii ya Watanzania. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
|
Sambamba na kuzibainisha changamoto wanazokabiliana nazo kama vitabu, madaftari,magodoro na sehemu za kulala, msimamizi wa kituo Al-Hajji Hussein pia naye alikuwa na yake ya kusema. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
|
Ahmad Mustapha ni mmoja kati ya vijana wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
|
Shumbana Hassan ni mmoja kati ya watoto wa kike wanao lelewa na Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza akitoa shukurani zake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
|
Licha ya kuushukuru uongozi wa kituo kwa makaribisho mazuri Meneja Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi amesema kuwa msaada huo ni utaratibu wa Kampuni ya Airtel kurejesha kwa jamii yake. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
|
Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza, kilianzishwa mnamo tarehe 3/07/ 2012 kina jumla ya watoto 50 kinachowalea, wa kike wakiwa 14 na wakiume 36.
Watoto wa kiume wanaishi katika nyumba maalum msikitini hapo, nao mabinti wakiishi kwenye hisani ya nyumba za majirani waliojitolea. |
Shukuran...Aksante!!
|
No comments:
Post a Comment