Sunday, June 1, 2014

WAHARIRI NA WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA KISIWA CHA SAANANE JIJINI MWANZA

Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakitoka katika lango la ofisi za Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane tayari kuelekea kisiwani.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habariwakiwa katika boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha  TBC 1,Ben Mwaipaja akiwa ameshika jembe lake tayari kwa ajili ya kuchukua matukio.
Safari ilikuwa ni ya takribani dakika 15 hadi 20.
Hatimaye Watalii hao wa ndani wakafika katika Kisiwa cha Saanane.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakikaribishwa na Mwongoza Watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saanane Patricia Mtenga.
Safari ya kuelekea katika eneo la kuanzia ziara ya kitalii katika Hifadhi hiyo ikaanza.
Baadae Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakapata historia ya Hifadhi hiyo kutoka kwa Muongoza Watalii Fua Hamis.
Baadhi ya Wahariri wa habari na Waandishi waandamizi toka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo ya mhifadhi Fua Hamis(Hayupo Pichani)
Safar ya kutembelea maeneo mbalimbali katika hifadhi hiyo ikaanza.
Moja ya eneo ambalo liliwavutia Wahariri hao ni eneo hili ambalo unatazama Taswira ya Ziwa Victoria vyema.
Safari iliendelea.
Eneo hili linajulikana kama Jiwe la Kuruka na hapa Mkuu wa Idara ya Ikolojia na Ulinzi katika HIfadhi hiyo Donates Bayona namna ambavyo watalii wa ndani wamekuwa wakifurahia kupata Taswira za Mawinguni wakiwa katika Jiwe hilo.
Baada ya kupita katika maeneo mbalimbali Safari ya Kurudi ikaanza.
Wakati Safari ya kurudi ikiendelea bahati mbaya Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa TANAPA ,Ibrahim Mussa aliteguka mguu baada ya kukanyaga vibaya jiwe hali iliyopelekea kupatiwa huduma ya kwanza.
Baada ya kufikishwa katika eneo la Mapumziko ndiko kukafanyika taratibu za kupelekwa Hosptali kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hatimaye akapelekwa Hosptali.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa jijini Mwanza.

No comments: