Friday, June 27, 2014

Ukeketaji Wanawake ni Udhalilishaji – Waziri Sophia Simba

eketaji.Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania. 
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kabla ya kufungua rasmi mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.
Washiriki Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Washiriki Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.

SERIKALI imesema kitendo cha baadhi ya makabila kuendeleza mila za kuwakeketa wanawake na watoto ni ukatili mkubwa ambao umekuwa na madhara kiafya kwa anayetendewa. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba alipokuwa akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji nchini Tanzania unaofanyika kwa siku mbili katika Mkumbi wa Mikutano wa Kunduchi Hoteli. 

 Waziri Simba alisema ukeketaji ni udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike na umekuwa ukihatarisha maisha ya wahusika kwa matokeo ya vifo, vilema na maradhi kama vile fistula na magonjwa mengine hivyo kutaka kila mmoja kuungana kuupinga. Alisema kwa upande wa Serikali imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha inatokomeza mila hizo pamoja na ukatili mwingine wa kijinsia. 

 “Wengi hapa ni mashaidi wa madhara ya ukeketeji ikiwemo vifo, vilema na maradhi kama vile, fistula na mengineyo. Serikali inalaani na kukemea ukatili huu unaomdhalilisha mwanamke na kumletea madhara makubwa,” alisema Waziri Simba. Aidha alisema ili kupambana na hali Serikali imesaini mikataba mbalimbali ya kukabiliana na ubaguzi anuai hasa kwa wanawake na pia kuanzisha Dawati la Jinsia kila sekta kukabiliana na vitendo vya kikatili nchini. “…Serikali iliandaa na inatekeleza mpango wa taifa wa kuzuia na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (2001-2015) na mpango wa kitaifa wa kutokomeza ukeketaji (2001-2015)…,” alisisitiza Waziri Simba.

 Aliongeza pamoja na hayo na juhudi mbalimbali za Serikali ukatili huo kwa wanawake na watoto hauwezi kuzuiliwa kwa sheria na mipango ya serikali hivyo kuitaka jamii pamoja na wadau wengine kuunganisha nguvu kupambana na vitendo hivyo hapa nchini. “….Suala la kutokomeza ukatili wa kijinsia, halitakwisha kwa kutegemea Serikali au sheria peke yake. Ni jukumu letu wadau wote kwa pamoja kukemea na kupiga vita kwa nguvu zote, kutoa elimu dhidi ya ukatili, huduma kwa wahanga na kuhakikisha wanaotenda na kubariki vitendo hivi wanachukuliwa hatua,” alisema.

 Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Mwakilishi wa UNFPA Tanzania, Mariam Khan alisema licha ya juhudi zinazofanywa kupambana na ukeketaji nchini, kila mwaka vipindi vya ukeketaji bado wasichana na watoto wanaokeketwa wamekuwa wakipoteza maisha bila sababu ya msingi kutokana na madhara ya ukeketaji jambo ambalo haliwezi kuvumiliwa. Aliwataka washiriki kwa pamoja kujadiliana nini cha kufanya ili kukomesha ukatili huo unaoendelea kushamiri nchini na kuahidi kuwa UNFPA itaendelea kuunga mkono juhudi za mapambano hayo kwa kutoa mafunzo na kuwezesha shughuli za mapambano hayo.

 Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valerie Nsoka alisema mkutano huo umewashirikisha wakuu wa mikoa, viongozi wa dini, wawakilishi wa madawati ya jinsia na wadau wengine kutoka mikoa yenye vitendo vya ukeketaji pamoja na asasi zinazopambana na ukeketaji. Aliongeza kuwa mkutano huo utafanyika kwa siku mbili ambapo wajumbe, watapeana uzoefu na kufanya majadiliano ya kina kabla ya kuibuka na mpango kazi wa nini kifanyike kutokomeza vitendo vya ukeketaji nchini. Mkutano huo ulioratibiwa na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) umefadhiliwa na Shirika la UNFPA, Tanzania. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini unaofanyika Kunduchi Beach Hotel and Resort jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, akizungumza katika mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania.
Mwakilishi kutoka Asasi ya NAFGEM inayofanya kazi mikoa ya Manyara na Arusha akielezea namna shirika hilo linalofanya kazi. 
Mwakilishi kutoka Asasi ya NAFGEM inayofanya kazi mikoa ya Manyara na Arusha akielezea namna shirika hilo linalofanya kazi kwenye Mkutano wa Kitaifa wa Kujadili Utokomezaji wa Ukeketaji Nchini Tanzania. Mkaguzi wa Polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto, Tarime-Rorya, Saumu Ngoma akizungumza na wanahabari namna dawati hilo linavyoshiriki kupambana na vitendo vya kikatili ukiwemo ukeketaji. 
Mkaguzi wa Polisi, kutoka Dawati la Jinsia na Watoto, Tarime-Rorya, Saumu Ngoma akizungumza na wanahabari namna dawati hilo linavyoshiriki kupambana na vitendo vya kikatili ukiwemo

No comments: