Mratibu
wa shindano la Redd's miss Sinza 2014 Tinna Matutuna katikati
akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Meeda
Night Club sinza juu ya Shindano la Redd's Miss Sinza litakalofanyika
kesho ijumaa katika ukumbi wa Meeda Night Club kwa kiingilio cha 5,000
kwa viti vya kawaida na 10,000 kwa Viti Maalum .kushoto na kulia ni
baadhi ya warembo wa shindano hilo.
======= ====== =====
MNYANGE
atakayefanikiwa kuibuka mrembo wa kitongoji cha Sinza ‘ Redds Miss
Sinza 2014’ katika shindano litakalofamyika leo Ijumaa kwenye Ukumbi wa
Meeda Night Club uliopo Sinza jijini Dar es Salaam atazawadiwa kitita
cha Sh. 300,000.
Akizungumza
jana jijini, Mratibu wa shindano hilo, Tinna Makutika, alisema kuwa
mshindi wa pili atajinyakulia Sh. 200,000, mshindi wa tatu Sh. 100,000
huku warembo wengine waliobakia kila mmoja ataambulia zawadi ya kifuta
jasho ya Sh. 50,000.
Mratibu
wa shindano hilo alisema kuwa maandalizi ya kinyang’anyiro hicho
yamekamilika na anaamini Sinza mwaka huu itafanikiwa kutwaa taji la
taifa ambalo linashikiliwa na mrembo kutoka Dodoma.
Alisema
kuwa warembo wake wamejiandaa kuonyesha ushindani na kila mmoja
amejipanga kufanya vizuri ili kushinda taji la Sinza usiku wa leo.
"Mwaka
huu nina warembo wazuri na wenye vigezo vyote, naamini mwaka huu
nitarudisha heshima ya watu wa Sinza ya kufanikiwa kutoa mshindi wa
taji la Redd's Miss Kinondoni na Redd's Miss Tanzania mwaka 2014”,
alisema Tinna.
Aliongeza kuwa wamejipanga kuendeleza mazuri yaliyofanywa na Brigitte
Alfred, ambaye alitwaa taji la taifa na kupata nafasi ya kuitangaza
nchi kwenye mashindano ya dunia ya Miss World.Alisema pia shindano hilo
linatarajiwa kuwa na burudani mbalimbali ikiwamo bendi mahiri ya muziki
wa dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambao wanatamba na Chuki ya
Nini. Kiingilio cha juu katika shindano hilo ni Sh. 10,000 kwa viti
maalum na vya kawaida ni Sh. 5,000.
Aliwataja
warembo 12 watakaochuana ni Liliani Sandi,Priscar Sarakikya,Agnes
Mwikombe,Esta Wilson,Rose Lucas,Zubeda Saburi,Tuku Harison,Dorine
Benne,Farida Iddy,Qeenlatifa Hashim,Jane Masawe na Wahida Ahmed.
Naye
Meneja wa kinywaji cha bia ya Redd’s Original, Victoria Kimaro, alisema
ni muda muafaka kwa wapenzi wa tasnia ya urembo nchini wanatakiwa
kujitokeza kwa wingi kuhudhuria shindano hilo ili kushuhudia namna
kitongoji cha Sinza kilivyo na bahati ya kutoa warembo wenye ushindani
katika fainali za taifa.
Victoria
alisema kuwa wadau wa sanaa ya urembo wanatakiwa kuona sanaa hiyo ni
sehemu inayowapa nafasi wasichana kutimiza ndoto zao na hatimaye
kujiendeleza kimaisha.
No comments:
Post a Comment