Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwenye hoteli ya Oceanic Bay mjini Bagamoyo asubuhi hii wakati wa seina inayojadili masuala mbalimbali yakiwemo mafanikio ya mfuko huo, malengo na Changamoto zake katika kufanikisha huduma ya afya kwa jamii, ambapo uwigo wa walengwa katika huduma hizo umeongezeka kutoka kaya 120 mwaka 2009 na kufikia kaya 668.474 mwaka 2014 sawa na wanufaika milioni 4.01 na mpaka sasa mfuko huo unafanya kazi na Halmashauri za wilaya 129 katika nchi nzima kati ya Halmashauri 168 zilizopo lakini pia tayari Halmashauri 20 kati ya hizo zimeshahamasishwa na zitaingia katika mpango huo siyo muda mrefu, .(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-BAGAMOYO) Eugen Mikongoti Mkurugenzi wa Uendeshaji akitoa mada katika semina hiyo juu ya uchangiaji wa huduma za mfuko wa bima ya afya kulia ni Raphael Mwamoto Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti na katikati ni Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF)
Dk Frank Lekey Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Kitaaluma akitoa mada kuhusu uboreshaji wa huduma za mfuko wa Afya ya jamii ambapo kwa sasa wanafanya kazi na hospitali za serikali na baadhi ya hospitali za mashirika ya dini. Rehani Athman Kaimu Mkurugenzi wa \mfuko wa afya ya Jamii (CHF) akizungumzia mafanikio yaliyokwishapatikana kutokana na huduma za mfuko wa Afya ya jamii
John Bwire Mkurugenzi wa kampuni ya Raia Mwema na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbalzinazotolewa katika semina hiyo Kulia ni Mhariri Dany Mwaijega na wenzake wakifuatilia majadiliano ya semina hiyo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri mtendaji wa New Habari Bw. Absalom Kibanda akizungumza katika semina hiyo inayofanyika mjini Bagamoyo anayefuata ni Abdalla Majura kutoka ABM Radio. Mhariri wa Gazeti la Mawio Jabir Idrissa akitoa mchango wake wakati wa majadiliano katika semina hiyo Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya NHIF Khamis Mdee na viongozi wengine wa mfuko huo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa rasmi mjini Bagamoyo. Wahariri mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kufungua semina hiyo Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi na Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wakiwa katika picha ya pamoja. Kulia ni Anna Mhina Katibu Mhutasi katikati ni Hawa Diguza Afisa Masoko na Elimu kwa Umma na Anna Mziray Meneja wa Msoko na elimu kwa umma wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment