Monday, June 30, 2014

NHIF YATETA NA WADAU WAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM

1Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akifungua mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya NHIF uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Malimu Nyerere Conference Centre jijini Dar es salaam kuzingumzia mambo mbalimbali kuhusu huduma hiyo ya bima ya afya, wadau waliohudhuria katika mkutano huo n kutoka wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni mkoani Dar es salaam, Lengo kuu likiwa kuhamasisha na wananchi kujiunga na mfuko huo na kufikia asilimia 30% ifikapo mwaka 2015, Pia kuangalia changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa malengo hayo na kuzitatua.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2Kamimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Afya Bw. Khamis Mdee akizungumza na kuelezea mikakati ya mfuko huo kwa wadau waliohudhuria katika mkutano huo leo. 3Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Taifa Afya ya Jamii NHIF Balozi Ally Mchumo akimkaribisha mgeni rasmi ili kuzungumza na wadau wa mfuko huo. 4Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi kushoto akiwa katika meza kuu wakati wa mkutano huo kulia ni Jason Blasius Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Katikati ni Teresia Mbando Katibu Tawala mkoa wa Dar es salaam. 5Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamoto akiteta jambo na mmoja wa wadau wa mfuko huo. 6Baahi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo 7 8 9Mbunge wa jimbo la Kigamboni Dr. Faustine Ndungulile akiwa katika mkutano huo. 10Anjela Mziray (kushoto) Meneja masoko kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akisoma taarifa za mkutano huo ulipokuwa ukiendelea. 11Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi na viongozi wa mfuko huo wakipig picha na wadau mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo. 12 13 14 15Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Waya ya Ilala Mh. Raymond Mushi akihijiwa na vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kufungua mkutano huo

No comments: