Makamu wa Rais, Dr Bilal akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Wageni waalikwa katika kongamano.
Dubai, United Arab Emirates-Katika
kile kinachoonekana ni hatua kubwa katika kuelekea kutengeneza fursa
kwenye sekta ya uendelezaji wa makazi, Shirika la Nyumba la Taifa
limeweka historia kwenye soko la kimataifa na kufanikiwa kwa mara ya
kwanza kufanya kongamano la uwekezaji hapa Dubai ambalo limefanikiwa
kufikia lengo lake la kuonyesha fursa zilizopo kwenye sekta ya ujenzi
kwa makampuni makubwa ya ujenzi yaliyopo Mashariki ya Kati na
kwingineko.
Tukio
hili la kipekee na kihistoria kwa Tanzania lilizinduliwa na Makamu wa
Rais Mheshimiwa Gharib Bilal na lilihudhuriwa na makampuni makubwa ya
ujenzi Dubai kama Damac, Nahkeel, Jumeirah na Emaar, ambayo yamehusika
na ujenzi wa majengo makubwa na maarufu Dubai kama Burj Khalifa, Hoteli
za Jumeira na Dubai Mall.
Makampuni
mengine yaliyohudhuria kutoka ukanda wa Guba kama Qatar na Bahrain
pamoja na nchi nyingine kama Korea, Sweden na Romania yameonyesha kuwepo
kwa nia ya makampuni makubwa kuwekeza kwenye sekta ya makazi Tanzania.
1
1
Malengo ya Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa;
Kongamano
la Wawekezaji Wa Sekta ya Makazi Tanzania ni sehemu ya lengo kuu la
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Mchechu, ambaye
kwa sasa analiongoza shirika hilo kubwa Afrika Mashariki. Kipindi cha
Msechu kwenye uongozi kimeonyesha mabadiliko na ubunifu mkubwa kwenye
uendelezaji wa sekta ya makazi nchini.
Mchechu
anasema lengo kuu la kongamano hili ni hatua kubwa kuelekea mkakati wa
kuionyesha dunia kuwa Tanzania ni sehemu pekee likija swala la uwekezaji
na urudishaji wa faida kwenye sekta ya makazi.
‘Tanzania
inatoa fursa ya pekee linapokuja swala la uwekezaji kwenye sekta ya
makazi barani Afrika na hii ni kutokana na uwazi pamoja na utulivu wa
kisiasa na amani inayopatikana nchini, uchumi unaokua pamoja na
ushirikiano mkubwa unaotolewa na serikali’ anasema Mchechu.
‘Tukio
hili la kihistoria ni sehemu tu ya mpango kamili wa kuifahamisha dunia
kuhusu fursa za uwekezaji kwenye sekta ya makazi zinazopatikana nchini’
alisema Mchechu.
Mchechu
anaamini kuwa huu ni muda mwafaka kwa wawekezaji kuitazama Tanzania na
Afrika kwa ujumla. ‘Zamani ilikuwa ni hatari kwa wawekezaji kuwekeza
Afrika na Tanzania, lakini kwa uchumi wa leo, ni hatari kutokuwekeza
Tanzania’ alisema Mchechu.
Kati
ya miradi iliyoonyeshwa kwa wawekezaji ni pamoja na miradi mitatu
ambayo itaendelezwa kwa kwa kipindi cha miaka 5. Hii inajumuisha miradi
miwili ya kuendeleza Arusha inayoitwa Safari City na USA River ambayo
kwa pamoja itakuwa na jumla ya nyumba 8000, pamoja na mradi mwingine wa
kuendeleza makazi Dar es Salaam utakaofahamika kama Salama Creek
Satellite City ambao utakuwa na jumla ya nyumba 9,500.
Miradi
hii yote iko tayari kwa maana ya kuwa vibali vyote vya mradi
vimepatikana na kinachotakiwa ni kuwekeza tu, na ndio maana kongamano
hili lilikuwa muhimu kwa ajili ya kupata uwekezaji unaotakiwa.
Serikali inatimiza wajibu wake;
Makamu
wa Rais, Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wageni
waalikwa alielezea namna serikali yake imefanya kazi kubwa kwa miaka
michache iliyopita kuhakikisha inatengeneza fursa katika sekta ya
makazi, ambapo mabadiliko makubwa yalikuwa katika maeneo matatu makuu
ambayo sasa yamekuwa sheria. Maeneo hayo ni pamoja na mikopo ya nyumba,
uanzishwaji wa kampuni ya kusaidia kuwezesha mikopo ya nyumba
(TMRC),pamoja na upitishaji wa sheria ya Condominium ambazo kwa hakika
zimechangia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya makazi.
‘Tanzania
kwa sasa inashuhudia mafanikio makubwa kwenye sekta ya makazi, huku
kukiwa kuna upungufu wa jumla ya nyumba milioni 3.8 na upungufu huo
unakua kwa kiasi cha makazi 200,000 kwa mwaka, ambayo kwa hakika inatoa
changamoto kubwa kwa Tanzania lakini ni fursa kubwa kwa wawekezaji’
alisema Bilal.
Naye
Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Balozi
Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na wageni waalikwa alisisitiza namna
sekta ya makazi ilivyoimarika nchini Tanzania.
‘Sekta
ya makazi ndio sekta inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania na
tunakaraibisha wawekezaji kutoka nchi za falme za Kiarabu’ alisema
Mbarouk.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa George B.
Simbachawene, anasema msingi mkuu wa kukua kwa sekta ya makazi ni
ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi ambao unaruhusu uwekezaji
na ukuaji mzima wa sekta.
‘Ushirikiano
baina ya sekta binafsi na serikali ni muhimu kwa ukuaji wa sekta ya
makazi. Tukio kama hili linaruhusu wawekezaji kutoka nchi za falme za
Kiarabu kuona fursa zilizopo Tanzania na kuzitumia’ anasema
Simbachawene.
Kiwango cha Uwekezaji ni kipi?
Mchechu anasema kongamano la hili linalenga kufikia wawekezaji wenye uwezo wa kuanzia dola milioni 20 hadi dola nusu bilioni.
‘Tunajua
uwezo wa uwekezaji unaotakiwa hauwezi kufikiwa kwa usiku mmoja na ndio
maana miradi yetu mingi ni zaidi ya miaka 5 hadi 7, lakini tuna miradi
ambayo inaanzia dola milioni kumi hadi dola milioni mia, kwahiyo kiasi
chochote ambacho mwekezaji atakuwa nacho kati ya kiwango hicho tuna
fursa za kuwekeza’ anasema Mchechu.
Watanzania Wanaowekeza Tanzania:
Mchechu
anasema kutafuta wawekezaji hakuishii tu kwa wale walio nje ya Tanzania
bali hata kwa Watanzania, na kwa kuanza kutakuwa na kongamano mwisho wa
mwezi huu litakalofanyika Dar es Salaam ambalo litajumuisha wawekezaji
walio nchini wanaotaka kuendeleza nchi yao.
‘Hatujasawahau
dada na kaka zetu nyumbani Tanzania, wengi wao wana nafasi kubwa ya
kuwekeza katika miradi ya uendelezaji wa sekta ya makazi nchi, na
tunataka kuhakikisha wanapata fursa hiyo pia’ anasisitza Mchechu.
Ushirikiano na Wadau:
Kongamano
hili limefanyika kwa ushirikiano kati ya Balozi wa Tanzania Dubai,
Mheshimiwa Omary Mjenga pamoja na Balozi Maalumu wa Mambo ya Kiuchumi,
Bwana Cleophas Ruhumbika, ambao walishughulikia taratibu za kongamano
pamoja na kualika makampuni ya uwekezaji ya Dubai.
"Tuna
furaha kubwa kufanya kazi bega kwa bega na Shirika la Nyumba la Taifa
kwenye tukio hili la kihistoria’ anasema Mjenga. ‘ Sehemu kubwa ya kazi
yetu hapa Dubai ni kuwezesha fursa kwa Tanzania ambayo inaendana na
wajibu wetu hapa. Pia tuna furaha kubwa kuwa tukio limekuwa la mafanikio
makubwa na nina hakika kuwa fursa zaidi za wawekezaji kuja Tanzania
zitazidi kufunguka’ anamalizia Mjenga.
No comments:
Post a Comment