Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy,Brian Tracy kutoka nchini Marekani,akizungumza jambo mapema leo asubuhi katika moja ya ukumbi wa Serena Hotel,jijini Dar kuhusiana na semina maalum ya uongozi bora ilioandaliwa na Mikono Speakers iliyomuhusisha nguli huyo wa masuala ya uongozi na kutoka nchini Marekani na Azim Jamal pichani kulia ambaye ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.Wa pili kutoka kulia ni Wakurugenzi wa Mikono Speakers ambao ndio waandaji wa semina hiyo maalum ya Uongozi na kushoto ni (Deogratius Kilawe na Themi Rwegasira.
====== ====== =======
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Mikono Speakers wanakuletea semina maalum ya Ufanisi bora katika Uongozi itakayoongozwa na Nguli wa masuala ya uongozi na maendeleo, Brian Tracy kutoka nchini Marekani na Azim Jamal kutoka nchini Canada. Semina hii maalum chini ya nguli hao wenye kuheshimika duniani ni fursa ya kipekee kwa wa-Tanzania kujifunza na kuboresha vipaji vyao vya uongozi katika biashara na taasisi zao mbalimbali. Semina hii ya siku moja itafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam tarehe 13 ya Mwezi Juni, 2014.
Akiongelea kuhusu umuhimu wa Semina hii kwa umma wa Tanzania, mkurugenzi mkuu wa Mikono Speakers, ndugu Deogratius Kilawe aligusia kuhusu kukosekana kwa wa-Tanzania katika eneo la juu, hususani katika nyanja ya uongozi.
“Kama ukiangalia katika makampuni makubwa na taasisi mbalimbali hapa nchini, hasa maeneo ya uchimbaji madini, mawasiliano, huduma na taasisi za kifedha utaona kuwa ni wa-Tanzania wazawa wachache tu ndio wako katika ngazi za juu za uongozi. Ni asilimia nne tu, (4%) ya viongozi hao ni wazawa, na asilimia tisini na sita (96%) iliyobakia ni wageni.
Hali hii inabidi kubadilika kama kweli wa-Tanzania wanataka kuchukua hatamu ya uongozi na maendeleo yao,” alisema ndugu Kilawe. Semina hii inayoletwa na Mikono Speakers ni moja ya hatua na fursa za kuwafanya wa-Tanzania kuwa viongozi bora. Semina hii ambayo itaongozwa na nguli ambao wamefanya kazi na makampuni makubwa duniani, tuna imani itawawezesha wa-Tanzania kupata ujuzi wa kipekee katika kuboresha utendaji wao katika biashara, taasisi za umma na kijamii kwa ujumla,” aliongeza bwana Kilawe.
Semina hii inawalenga wale walio katika uongozi katika sekta binafsi, sekta za umma na taasisi za kijamii, kama makampuni ya umma, viongozi wa kiserikali, wabunge, wakufunzi na wote walio katika eneo la uongozi. Ni matarajio kwamba wadau mbalimbali kutoka makampuni makubwa, na makampuni ya kimataifa na taasisi ndogo na kubwa, wakiwamo na viongozi wakubwa wa kiserikali watahudhuria semina hii ya kipekee. Pia wananchi wote wanahimishwa kushiriki, haswa wale wenye kupenda kufahamu masuala ya uongozi.
Semina hii inadhaminiwa na:
· National Housing Corporation
· The Citizen Newspaper
· Dar Es Salaam Serena Hotel
· Julius Nyerere International Convention Centre
· Raha
· Montage Ltd
· Dephics Company Ltd
· Rodizio Brazilian Grill
· Dar City Promotions
· Prime Advertising
· Clouds FM
· Man Magazine
· Jamii Forums
· MICHUZI MEDIA GROUP.
Kuhusu waendesha Semina hii.
Brian Tracy
Brian Tracy ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy, kampuni inayayojihusisha na kutoa mafunzo kuendeleza watu na taasisi mbalimbali. Lengo la ndugu Tracy ni kuendeleza na kusaidia walengwa kufikia malengo binafsi na a kibiashara mapema zaidi.
Brian Tracy amesaidia zaidi ya makampuni 1000, na kuongea na watu zaidi ya milioni tano katika nchi arobaini (40) duniani. Ndugu Tracy amesoma, kufanya utafiti, na kuandika matoleo mbalimbali katika Nyanja za Uchumi, Biashara, Falsafa an Saikolojia. Ameandika zaidi ya vitabu 45 ambavyo vimetafsiriwa katika lugha mablimbali.
Azim Jamal
Azim Jamal ni mwazilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.
Ni mwandishi wa vitabu mbalimbali, vikiwamo “The Corporate Sufi”, “Business, Balance & Beyond” na pia ni mwandishi mwenza wa “The Power of Giving”. Ameshika nafasi ya kwanza katika mtadao wa Amazon wa mauzo ya vitabu mara mbili, 2005, na 2008, na pia ameshika nafasi hiyo katika kampuni ya Barnes & Noble.
Barnes & Noble ni muungano wa maduka makubwa zaidi duniani, yakimiliki maduka yapatao 3000. Vitabu vyake vimetafsiriwa katika lugha 10. Azim ana shahada tatu za mahesabu, na baada ya kufanya kazi na wakimbizi wa Afghanistan alibadilisha taaluma yake kutoka “mahesabu kwa biashara” kwenda “mahesabu kwa maisha” baada ya kuona maswaibu wayapatayo wakimbizi hao ambayo yalimgusa sana.
Ametoa ukufunzi kwa wamiliki wa makampuni ambayo ni ya thamani ya mabilioni ya dola. Wateja wake ni pamoja na “Fortune 500”, wanamichezo maarufu, na mengine mengi. Kwa kawaida katika mihadhara yake amekua akipata wastani wa alama 9+ chini ya kumi.
Ujumbe wake wenye kuvutia, kutoa hamasa, na wakati mwingine wenye mtizamo tofauti umeonwa na zaidi ya hadhira ya watu milioni moja katika nchi 26. Ujumbe wake kupitia vyombo vya habari umesikiwa na watu wapatao milioni 5. Amezaliwa Tanzania na anaongea Kiswahili.

1 comment:
Mikono nawatakia kila la kheri
Post a Comment