Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imekusudia kuongeza nguvu za ziada katika kusaidia kuimarisha miundo mbinu ndani ya Bara la Afrika kwa lengo la kuyajengea uwezo wa uzalishaji wa kiuchumi Mataifa mbali mbali yaliyomo ndani ya Bara hilo.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa China Bwana Li Yuanchao wakati yeye na ujumbe wake alipofanya mazungumzo Rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiuongoza Ujumbe wa Zanzibar kwa Niaba ya Rais wa Zanzibarna Mwenyekiti wa Bararaza la Mapinduzi Dr. Ali Moh’d Shein hapo hoteli ya La gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bwana Li Yanchao akiwa Zanzibar kwa siku moja akiendelea na ziara yake ya siku sita Nchini Tanzania alisema katika utekelezaji wa azma hiyo China imejipangia kutumia Yuan Bilioni 2.2 katika mipango yake ya kuimarisha miundo mbinu hiyo ya uwekezaji kwenye sekta ya biashara.
Aliishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuitumia fursa hiyo adhimu kwa kuchagua miradi yake itakayoipa kipaumbele cha kwanza kwa kuwasiliana na Ofisi ya Ubalozi mdogo wa Nchi hiyo uliopo Zanzibar ili kuratibu miradi hiyo na hatimae hatua za utekelezaji zianze mara moja.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa shukrani zake alisema Zanzibar itaendelea kuiheshimu na kuithamini China kutokana na msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za kuimarisha uchumi.
Balozi Seif alieleza kwamba Jamuhuri ya Watu wa China inastahiki kupongezwa kwa misaada yake mikubwa inayotoa kwa Zanzibar ambayo haijawahi kutokea katika Historia ya Zanzibar tokea Mapinduzi ya Mwaka 1964.
Alisema Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakishuhudia misaada tofauti inayotolewa na China ndani ya kipindi cha miaka 50 tokea Mapinduzi iliyolenga katika sekta za afya, elimu, maji, miundo mbinu, kilimo pamoja na mawasiliano.
Bwana Christopher Mush Smith wa Hoteli ya La Gema akikata Keki Maalum yenye Bendera za Tanzania na China iliyoandaliwa na Hoteli hiyo kwa ajili ya Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Li Yuanchao aliyepo pembeni yake akiwa sambamba na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao akipongeza na Mwenyeji wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya mazungumzo yaop yaliyofanyika katika Hoteli ya La Gema Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif na Mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao wakitoa nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyoshirikisha viongozi wa ngazi za juu wa pande zote mbili.
Bwana Li Yuanchao upande wa kushoto alinyanyuka na kufurahia muziki murua uliokua ukiporomoshwa na Kikundi cha taadab asilia cha Akheri Zamani wakati wa tafrija yao kwenye Hoteli ya La Gema Nungwi.
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ukiendelea na mazungumzo yao na ujumbe wa China chini ya Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao hapo katika ukumbi wa Hoteli ya La Gema Nungwi.
Ujumbe wa Zanzibar ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ukiendelea na mazungumzo yao na ujumbe wa China chini ya Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao hapo katika ukumbi wa Hoteli ya La Gema Nungwi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akimkabidhi Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao zawadi ya kasha kama kumbu kumbu ya ziara yake hapa Zanzibar mara baada ya kumaliza mazungumzo yao huko Nungwi.
Balozi Seif na mgeni wake Makamu wa Rais wa China Bwana Li Yuanchao wakifuatilia muziki laini wa kikunci cha taarabu asilia cha Akheri Zamani hakipo pichani kwenye tafrija yao hapo La Gema Nungwi.
Ukumbi wa Hoteli ya La Gema Nungwi iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ulisheheni vionja vya muziki wa Taarab asilia ya kikundi cha Akheri Zamani wakati wa tafrija maalum kwa ajili ya ugeni wa Serikali ya China uliooongozwa na Makamu wa Rais wa Nchi hiyo Bwana Li Yuanchao.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment