Mabingwa watetezi Bilele FC wameanza kwa kufungua Michuano hii ya Kagasheki Cup vibaya baada ya Kutandikwa bao 3-1 na Timu ya Rwamishenye Fc leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba Mjini. Bilele FC ndio walioanza kuifunga timu ya Rwamishenye katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza, Bao likifungwa na Miraji Ramadhan.
Kesho Mtanange unaendelea na utazikutanisha timu za Bakoba na Kashai, Mtanange utakao pigwa saa 10:00 jioni. Jumatatu kutakuwepo na mitanange 2 wa saa 8 na saa 10 jioni.
Wachezaji wa Rwamishenye Fc wakishangilia moja ya bao lao
Wachezaji wa timu ya Bilele Fc wakishangilia bao lao la dakika ya 5 lilifungwa na Miraji Ramadhan
Kikosi Cha Timu ya Rwamishenye kilichoanza
Kikosi cha Timu ya Bilele FC
Timu zikisalimiana
Waamuzi na Timu Kapteni timu zote mbili wakilianzisha
Waamuzi wa Mtanange huu
Kikosi cha Timu ya Rwamishenye uwanjani wakiomba kabla ya kipute kuanza muda mfupi
Mgeni Rasmi akisalimia timu ya Rwamishenye
Mgeni Rasmi akisalimia timu ya Bilele Fc ambao ndio Mabingwa watetezi wa Kombe hili
Mgeni Rasmi akiteta jambo na Wachezaji Pande zote mbili
Mashabiki wakishangilia timu yao
kipute kikiendelea..kaitaba
Wachezaji wa Timu ya Bilele walivalia jezi zinazofanana na Mbeya City
Patashika za hapa na pale zikiendelea, kila mchezaji akitaka aupate mpira
Kila Mchezaji alikuwa na mwenzake wakubanana nae.
Hapa ukatizi ndugu yangu!
Wachezaji wa Timu ya Rwamishenye wakicheza muziki baada ya kusawazisha
Mashabiki ndio usiseme...walifujaa uwanjani Kaitaba
Mashabiki
Waamuzi wakina Dada nao walikuwepo wakitazama wenzao wakiendesha mpira
Mchezaji wa Rwamishenye akishangilia bao lake la pili lililofungwa na Yahaya
Wachezaji wa Rwamishenye wakishangilia bao lao baada ya kuwanyuka Bilele Fc
No comments:
Post a Comment