Mjumbe
wa Kamati ya Urasimishaji wa Kazi za wasanii wa Filamu na Muziki hapa
nchini ambaye pia ni Afisa kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Wilhad
Tairo akifafanua jambo kwa mfanyabiashara wa duka la Filamu wakati wa
Operesheni ya kukagua Bidhaa zisizo kuwa na Stempu za TRA, Operesheni
hiyo ya wiki mbili iliyoanza jana jijini Dar es Salaaminatekelezwa kwa
uhirikiano wa TRA, Bodi ya Filamu, Basata na Cosota
Mfanyabiashara
wa duka CDs za Filamu lililopo maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam
akieleza jambo kwa maafisa wa Kikosi kazi kwa ajili yakukagua bidhaa
ambazo azizingatii taratibu kabla ya kuingizwa sokoni leo jijini Dar es
Salaam.
Muuzaji
wa duka la CD za Filamu katika mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam
akiwaonyesha Stempu za TRA katika CD zake wakaguzi kutoka TRA,Bodi ya
Fila, Basata na Costa ambao walifika dukani kwake kwa ajili ya ukaguzi
wa bidhaa ambazo zimeingizwa sokoni bila kufuata taratibu za kisheria
iliwemo kuweka Stika za TRA kama sheria inavyotaka.Kamati ya
urasimishaji wa kazi za wasanii wa Filamu na Muziki wameanza Operesheni
ya wiki mbili katika jiji la Dar es Salaam ili kuleta ufanisi katika
mapato ya Wasanii.
Afisa
Kodi Msaidizi Bi. Theophilda Majara( Mwenye blauzi nyekundu) akikagua
uhalisi wa Stempu za TRA katika CD za Filamu leo jijini Dar es Salaam
wakati wa Operesheni ya kukagua na kukamata Filamu zitakazo kuwa
hazijafuata utaratibu wa kisheria wa kuweka Stika na kusajili katika
mamlaka husika.
Mfanyabiashara
wa duka la CDza Filamu nchini akisoma kanuni za stempu za bidhaa za
Filamu na Muziki zilizo china ya sheria ya ushuru wa bidhaa
walipotembelewa na Kikosi kazi kinachofanya Operesheni ya kukagua bidhaa
hizo ambazo zimeingia sokoni bila kuzingatia taratibu na matakwa ya
sheria hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa
Kodi Msaidizi Bi. Theophilda Majara( Mwenye blauzi nyekundu) akikagua
baadhi ya CD za Filamu wakati wa Operesheni ya kukagua Filamu ambazo
hazijafuata taratibu za kisheria ikiwemo kulipia Stempu ya TRA kabla ya
kuingia sokoni. Zoezi hilo linaendeshwa kwa ushirikiano wa TRA, Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Bodi ya Filamu, Basata
na Costota .
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia namna Operesheni ya kukagua Filamu zilizoingia
sokoni bila kufuata utaratibu namna inavyotelekelezwa jana katika mitaa
ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija
No comments:
Post a Comment