Thursday, May 15, 2014

WAKULIMA WA TUMBAKU WAULALALMIKIA UBADHILIFU MKUBWA WA FEDHA ULIOFANYWA NA VYAMA VYA USHIRIKA WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA.

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia,wakazi wa Sikonge katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,wilayani Sikonge mkoani Tabora.Kinana alizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakumba wakulima wa zao la Tumbaku huku akionesha kabrasha la taarifa ya ukaguzi na uchunguzi wa chama cha Ushirika cha WETCO LTD,ambalo linaeleza namna wakulima wa Tumbaku walivyoibiwa mamilioni ya fedha.

Aidha,Wananchi wa Sikonge wameulalamikia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha uliofanywa na viongozi wa vyama vya ushirika,Kufutia taarifa ya ukaguzi na uchunguzi katika vyama hivyo vya ishilika,inaelezwa kuwa kiasi cha fedha milioni 28 zimefujwa,na kwamba wamekuwa wakicheleweshewa malipo ya fedha zao na pia kutolipwa kwa wakati,jambo ambalo limekuwa likiwakera wakulima hao na kuwarudisha nyuma katika suala zima la  maendeleo.

Kinana aliongeza kusema kuwa vyama vya ushirika vimeanzishwa kwa wingi na wajanja wachache kwa ajili ya kujinufaisha wao na kuwanyona na kuwadhuruma wakulima wa Tumbaku,hivyo Kinana alisema kuwa amekisikia kilio cha wakulima hao,na ameahidi kuyafikisha malalamiko hayo kwa Rais Jakaya Kikwete na hatimaye kupatiwa ufumbuzi. 
 Wakazi wa mji wa Sikonge wakiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa CCM,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowahutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa Sikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM,mkoani Tabora.
Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye,akiwahutubia mamia ya wakazi wa mji wa Sikonge waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa CCM,Wilayani humo mkoani Tabora.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Sikonge,Said Mkumba kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakumba wakulima wa zao la Tumbaku wilayani Sikonge mkoani Tabora,ambapo inaelezwa kuwa wakulima hao wamekuwa wakilaghaiwa,kudhulumiwa na kunyonywa na vyama vya ushirika huku ubadhilifu mkubwa wa fedha ukifanywa na vyama hivyo.
Mbunge wa jimbo la Sikonge,Said Mkumba akiwahutubia wananchi wa sikonge mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongezana na Mkuu wa Mkoa,Mh,Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,siasa na Uenezi Nape Nnauye wakikagua mradi wa ufugaji kuku wa asili ikiwa ni sehemu ya mradi wa Vijana wa Path Finder Green City,Wilayani Sikonge mkoani Tabora.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiongozwa kwenda kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Mazinge wilayani Sikonge,kituo hicho kitakuwa kinatoa huduma mbalimbali kama vile wagonjwa wa nje,kuhudumia Wazazi na watoto,waja wazito,sehemu ya kuhifadhia maiti,Wodi ya Wanaume na nyinginezo.
Mkufunzi wa Kilimo cha Tumbaku kutoka kampuni ya TLTC,Goodluck Mmasi akifafanua namna ya uhifadhi tumbaku kwenye maghala  na namna inavyochambuliwa,Mradi huo ni wa Vijana wa PathFinder Green City,ambao wamekuwa wakijituma kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo na za ujenzi pia katika suala zima la kujikwamua na umasikini.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Vijana wa PathFinder Green City,katika kata ya Pangale Wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Sehemu ya mradi wa Vijana wa Ufugaji Nyuki katika kijiji cha Path Finder Green City kilichopo katika kata ya Pangale,wilayani Sikonge mkoani Tabora,Vijana hao wana jumla ya Mizinga ya nyuki 600 maalum kwa ufugaji nyuki.

PICHA NA MICHUZIJR-SIKONGE TABORA.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

No comments: