Thursday, May 29, 2014

VIONGOZI WASIOTIMIZA WAJIBU WAO MKOA WA MANYARA KUBURUZWA KWA RAIS - KINANA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akilakiwa   kwa shangwe alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango katika Jimbo la Babati Vijijini, mkoani Manyara. Kinana yupo mkoani Manyara kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Tayari kafanya ziara hiyo katika mikoa ya Tabora na Singida.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati) akilakiwa   kwa shangwe alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango katika Jimbo la Babati Vijijini, mkoani Manyara. 

 Wananchi wa Kijiji cha Ayamango, Babati Vijijini wakiwa na bango la asili lenye maandishi yanayosisitiza umuhimu wa kuendelea na Muungano wa Serikali mbili badala ya tatu.
 Wazee wa Kijiji cha Ayamango wakimvisha mgolole,Kinana ikiwa ni heshima ya kuwa mmoja wa wazee wa kijiji hicho.
 Wanachama wa CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho wakati wa mkutano huo wa hadhara.

 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango, Babati Vijijini. ambapo alikerwa kwa kiasi kikubwa na jinsi wananchi wanavyoporwa maeneo yao na viongozi wa chama na Serikali ambapo aliahidi suala hilo kulitafutia ufumbuzi kwa kulipeleka katika vikao vya juu vya chama hicho.
 Kinana akiwasikitishwa jinsi wananchi vijijini wanavyoporwa ardhi na kutumia mahakama kuchelewesha haki zao
.Kinana amesema kuwa viongozi wasiotimiza wajibu wao Mkoa wa Manyara atawaburuza kwa Rais.

 Vijana wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za umoja wa vijana wa CCM kwenye mkutano huo
 Wananchi wakiwa na bango linalosisitiza kendelea na mfumo wa Serikali mbili badala ya tatu
Kikundi cha vijana kikitumbuiza wakati wa msafara wa Kinana ulipowasili katika Kijiji cha Ayamango.

 Kinana akipandisha bendera ikiwa ni ishara ya kuzindua Tawi la CCM la Ayamango, Babati Vijijini.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ayamango na kuwaambia wananchi kuachana kabisa na wapinzani akidai tayari vyama vyao vimeanza kufa na haviwaletei maendeleo kama ilivyo CCM inayojali maisha ya Watanzania. 

No comments: