JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anwani ya Simu: POLISI
TABORA
Fax: 026 – 2605489
Nambari za Simu: 026 – 2605478
Unapojibu tafadhali taja.
|
|
Ofisi ya:-
KAMANDA WA POLISI MKOA,
S.L.P. 23,
TABORA.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 26/05/2014.
Ndugu
waandishi wa habari, Jeshi la Polisi mkoa wa Tabora linaendelea na Operesheni katika
wilaya zote za mkoa wa Tabora. Ambapo kufuatia operesheni hiyo tumefanikiwa kukamata
:-
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA ASKARI:
Katika
mwendelezo wa upelelezi wa matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha
hapa mkoani Tabora walikamatwa
watuhumiwa saba waliohusika na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha na mauaji ya askari Na.F.5179 Pc Jumanne
na G.3388 Pc Shabani huko Usoke Wilaya ya Urambo.Watuhumiwa hao ni:
1.SILVESTER s/o MUSSA @
KINGWENDU @TAMATI 31yrs mkazi wa Mkuyuni Tambukareli – Mwanza
2.SADIKI s/o HAMISI RUSHIKAMWA
@SADICK MILAMBO @WHITE
28yrs
mkazi wa Mihogoni –Tabora
3. ABEL
S/O BENEDICT @MWENDO WA SAA 23yrs Mfipa mkazi wa Urambo Muungano
4. FRANCIS S/O KASHINJE @MASANJA 38yrs
Msukuma, mkazi wa Nansio – Ukerewe
5. HAJI
S/O ATHANAS @SIMBA,50yrs Mnyamwezi Mkazi wa Usoke
6. MUSSA
S/O KHATIBU ALLY@MUSSA BONGE,49yrs Mnyamwezi Mfanyabiashara wa Nafaka na mkazi
wa Mwanza Rd.
7.RAMADHANI
S/O KASSIM MKUNYA@RAMA MANYWELE@RAMA MREFU Mkazi wa Tabora
Baada ya
mahojiano nao walikiri kushiriki matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia
silaha likiwemo tukio la tarehe 28/04/2014 katika tarafa ya usoke ambalo
lilipelekea kuuwawa kwa askari wawili. Baada ya kupekuliwa walipatikana na
silaha Pistol Glock17 namba TZ Car 91968
ikiwa na magazine yenye risasi tano.Aidha
katika Msako unaoendelea huko Urambo tarehe 25/05/2014 majira 0200hrs
alikamatwa mtuhumiwa mmoja na silaha aina ya gobore iliyotengenezwa kienyeji
ikiwa imekatwa kitako na risasi 2 za shortgun na 3 za SMG/SAR,upelelezi
unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi
kukamilika.
KUKAMATWA WATUHUMIWA 10 KOSA LA KUPATIKANA
NA BHANGI MAGUNIA SITA NA KETE 402:
Katika
hatua nyingine msako uliofanyika huko Wilaya ya Kaliua, Nzega na Tabora
Manispaa wamekamatwa watuhumiwa
wa kumi
msukuma
wakiwa na gunia 6 za bhangi na kete 402.
1. PINGWA s/o BUHILA, 14yrs, msukuma,mkazi
wa mpandamlowoka
2. MAGRETH d/o JULIUS, 15yrs,
msukuma mkazi wa mpandamlowoka
3. MALALE s/o KWANGULIJA, 13yrs,
msukuma,mkazi wa mpandamlowoka
4. HALIMA d/o MIHAMBO, 70yrs,
5. HASANI s/o HASANI, 40yrs,
6. MRISHO s/o JUMA, 33yrs,
M/mwezi, Mtaturu, mkazi wa azimio Isevya,
7. GEORGE s/o BALTAZARI, 31yrs,
msukuma
8. BAMKUBWA
s/o
MOHAMEDI
49yrs
mgogo,
PAULO
s/o BUNDALA,
33yrs, Msukuma
9. JUMA s/o SHIJA, 28yrs, Mnyiramba,
Watuhumiwa
watatu ambao wana umri mdogo rbada ya kuhojiwa walikiri kufanya biashara ya
uuzaji wa bhangi ambayo hutumwa na wazazi wao aidha watuhumiwa wengine wamekiri
kuwa ni wauzaji wa bhangi. Wazazi wa watoto hao wanatafutwa na Jeshi la Polisi na
watafikishwa mahakamani mara moja.
KUPATIKANA MITAMBO YA KUTENGENEZEA POMBE MOSHI:
mnamo tarehe 21/05/2014 huko eneo la ng’ambo kata ya Ng’ambo manispaa ya Tabora
alikamatwa CHAUSIKU d/o
ABDALA, 38yrs, M/mwezi, mkazi wa Ng’ambo
akiwa na mitambo 5 ya kutengenezea pombe ya moshi,baada
ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kuwa ni mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo.
Mtuhumiwa amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zake.
KUKAMATWA WATUHUMIWA 8 NA LITA 110 ZA POMBE YA MOSHI:
Huko Wilaya
ya Igunga na Sikonge 8 na jumla ya lita 110 za pombe ya Moshi,watuhumiwa
waliokamatwa ni pamoja na:
1. MWAJUMA
d/o SALEHE, 45yrs, mnyaturu, mkazi wa mwanzugi
na
2. ALLY s/o MUSA, 24yrs, muha,
3. KATALINA
d/o AMOUR,
4. MAERRY
d/o LUKAS
5. EMMANUEL
s/o KILASA, 29YRS M/MWEZI,
6. CATHERINE
D/O MPALASINGE,50yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
7. MARIA
D/O DAUDI 24yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
8. KAUMBWE
S/O IBRAHIM 26yrs MNYAMWEZI MKAZI WA USUKILO SIKONGE
Watuhumiwa
ni wauzaji na watumiaji wa pombe hiyo.watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani.
AJALI YA MOTO KUSABABISHA KIFO: Mnamo
tarehe 21/05/2014 huko kijiji cha Mwanzugi, kata/tarafa na wilaya ya Igunga
moto uliwaka kwenye chumba cha kufanyia biashara ya mkaa katika nyumba ya NTEJO
s/o ZANZIBAR,
42yrs, Msukuma, mkazi wa Mwanzugi na kusababisha kifo cha DORA
d/o BUNDALA,
35yrs, Msukuma, mkazi wa Mwanzugi na majeruhi mmoja ambaye anapatiwa matibabu
katika hospitali ya wilaya ya Igunga. Chanzo cha moto huo marehemu alikuwa
anapika katika jiko la mkaa huko ndani ya nyumba kukiwa na madumu yaliyokuwa na
petrol na kusababisha mlipuko huo. Mmiliki wa nyumba hiyo alitoweka mara baada
ya tukio hilo na kwenda
kusikojulikana. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.
KUKAMATWA KWA GARI LINALOSADIKIWA KUWA LA WIZI
Mnamo
tarehe 25/05/2014 majira ya saa 1830hrs huko maeneo ya Kanyenye Kata ya
Kanyenye Manispaa ya Tabora alikamatwa Moses S/O Meshack 37yrs Muha ,Mkazi wa
Ipuli akiwa na gari namba T 636 DUW Toyota Harrier rangi ya Metalic Silver,Chassis
No.100078234,Engine
No.1MZX 0986347 ambalo alishindwa
kulitolea maelezo.Uchunguzi wa awali unaonesha gari hilo mmiliki halali ni
Bw.Abrahamu S/O Joseph Myahucho mkazi wa Dar Es Salaam.Upelelezi unaendelea
kuhusiana na uhalali wa gari hilo.
Jeshi
la Polisi mkoa wa Tabora linazidi kutoa rai kwa wananchi kuzidi kushirikiana
nasi katika kupambana na uhalifu na wahalifu kwa kutoa taarifa zitakazowezesha
kubaini uhalifu na kuwakamata.Aidha kufuatia matukio ya moto tunatoa wito kuacha
tabia ya kuhifadhi mafuta hasa ya Petrol/|Diesel ndani ya nyumba kwani kwa
kufanya hivyo wanahatarisha usalama wao na mali zao.
Imetolewa
na :-
Suzan S. Kaganda
-ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA TABORA.
No comments:
Post a Comment