Mtaalamu wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya kukodi.
McClements akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena ndege yake kuelekea jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Dr. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Ili chukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 tu maji yalikuwa yameishatoweka
Akipima maji aliyoweka
No comments:
Post a Comment