Tuesday, May 27, 2014

MAMA SHEIN aongoza hafla ya kukubidhi madawati Skuli ya Msingi Mgenihaji Zanzibar

DSC_0768
MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Unguja Mhe. Mahammed Raza, akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakatin wa kukuabidhi madawati kwa Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja.jumla ya madawati 100 na viti 100 vimekabidhiwa skuli hiyo jana.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0774

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi  Madeski Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mgenihaji Ndg.Ali Mohammed Nassor, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya skuli ya Mgenihaji kulia Mwakilishi wa Uzini Mhe. Mohammed Raza madawati hayo yametolewa na Ndg Abdulhamid Mohammed Ali Mhoma, kupitia kwa Mwakilishi wa Uzini Mhe Mohammed Raza..(Picha Othman Maulid)
DSC_0786

WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia katika hafla ya kukabidhi madawati kwa ajili ya skuli hiyo.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0829 

MWALIMU Fatma Suleiman, akisoma risala ya Wananchi wa Mgenihaji wakati wa hafla wa kukabidhi madawati yaliotolewa na Mhe Mohammed Raza kwa ajili ya Skuli ya Msingi ya Mgeni haji Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0845

MKE wa Balozi wa Mdogo wa China Zanzibar Bi Wu Yan, akiwasalimia Wananchi na Wanafunzi wa Mgenihaji wakati wa hafla ya kukubidhi madawati na Vifaa mbalimbali kwa Wanawake wa Mgenihaji.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0853 

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Jimbo la Uzini Unguja wakati wa hafla ya kukubidhi Vifaa kwa ajili ya Vikundi vya Ushirika na Madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji, kulia Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt Idris Muslim Hija na kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Seif.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0875 

MWAKILISHI wa Jimbo la Uzini Mhe Mohammed Raza, akimkabidhi zawadi Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati ya Skuli ya Msingi Mgenihaji Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Othman Maulid)
DSC_0893

MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi Vyarahani Viwili, Nyuzi na Vitambaa. Kiongozi wa  Kikundi cha Kasi Mpya.Ndg. Mwanaisha Mtumwa.(Picha na Othman Maulid)  

No comments: