Saturday, May 17, 2014

KINANA AITAKA SERIKALI KUWAPELEKA MAHAKAMANI VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA WALIOTAFUNA FEDHA ZA MALIPO YA WAKULIMA WA TUMBAKU TABORA

 Fulana iliyovaliwa na Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Athuman Kapuya ikiwa na maandishi ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana wilayani Kaliua, Tabora leo.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kaliua na kuitaka serikali kuwacvhukulia hatua za kisheria watu wote walishiriki kuwaibia fedha wakulima wa tumbaku mkoani Tabora.Kinana yupo mkoani Tabora kwa ziara ya siku 11 ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuta Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG


 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kaliua leo, ambapo alisema kuwa viongozi wa Ukawa kwa tabia yao ya uchonganishi na fitina zao kwa wananchi ni kufilisika kisiasa.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM mjini Kaliua leo. Aliema kuwa ili kupunguza dhuluma kwa wakulima wa tumbaku, wakulima kuanzia sasa wameruhusiwa kuuza zao hilo kwa watu binafsi na vyama vya Ushirika mkoani humo.
 Wananchi wakishangilia kwa kumuita Jembe Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Kaliua.
 Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi, Athuman Kapuya akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuelezea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya CCM.
Kinana akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakati wa mkutano wa hadhara mjini Kaliua.

No comments: