Kundi la watalii wa ndani ambao minongoni mwao walikuwa ni Askari kutoka chuo cha taaluma ya Polisi Moshi wakipanda kuelekea Shira Hut moja ya kilele katika Mlima Kilimanjaro. |
Ofa ya utalii wa ndani katika mlima Kilimanjaro ilijumuisha watu wa Kila Rika,hapa mmoja wa watalii wa ndani akiwa na mtoto wake mgongoni. |
Kiasi safari ilikuwa ngumu kwa baadhi ya watalii wa ndani |
Kila hatua zilizo pigwa wataalii wa ndani walipenda kuchuku Taswiras. |
Na safari iliendelea hapa ikiongozwa na mkufunzi mkuu wa chuo cha polisi Moshi ,SSP,Grayfton Mushi. |
Baadhi ya watalii walionekana kuchoka lakini kila walipoulizwa walidai wameweka pozi la picha. |
Safari ya baba na mwana iliendelea ,Mgongoni ni Mtoto Matinde Chacha akiwa na baba yake John Chacha. |
Hatimaye watalii wakafika Shira Hut,wengine wakiwa wametupia mavazi ya Suti. |
Afande akiwa hoi baada ya safari ya saa moja ya kufika Shira Hut. |
Waliofika wakafurahia madhari nzuri na kupata Taswira ya pamoja. |
Safari ya kuelekea katika mapango ya Shira(Shira Caves)ikaanza tena kutoka Shira hut. |
Mkuu wa mafunzo katika chuo cha taaluma ya Polisi ,Grayfton Mushi akipozi huku mwenzake Moses Ruvinga ambaye pia ni afisa katika chuo hicho akichukua taswira. |
Baadhi ya watalii wa ndani wakiwa ndani ya moja ya Mapango ya Shira yaliyoko katika mlima Kilimanjaro. |
Watalii wa ndani wakiwa katika eneo hilo la Mapango. |
Watalii wa ndani wakatembelea eneo la Shira Camp kujionea watalii wanavyo lala wakati wakifanya safari ya kuelekea katika kilele cha Kibo . |
Hapo wakakutana na Wabebaji wa mizigo ya watalii maarufu kama Wagumu na kupata nyinmbo mbalimbali. |
Waliopanda na vazi la Suti wakaonesha vipaji vyao vya kusakata Kiduku, |
Wengine walipata fursa ya kupiga picha na watalii waliokuwepo katika kituo hicho. |
Kutokana na kuchoka wengine waliamua kupumzika katika machela maalum ya kushushia watu waliozidiwa mlimani. |
Baadae safari ya kurudi toka mlimani ikaanza. |
1 comment:
It was very nice.....Tumefurahia sana hiyo safari
Post a Comment