Tuesday, April 29, 2014

Vodacom yawaunganisha Buhigwe kwenye mtandao wa simu za mkononi

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom kuashiria kuanza kupatikana huduma za kampuni hiyo ya simu nchini katika kijiji cha Bukuba kilichopo Buhigwe mkoani Kigoma. Pembeni yake ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Malcelina Mbehoma na Mwenyekiti wa Halmashauri Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Charles Gishuli (mwenye koti) akitumia simu yake ya mkononi kutuma fedha kupitia huduma ya M-pesa mara tu baada ya kuzindua huduma za Vodacom katika kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli jinsi ambavyo wakazi wa kijiji cha Bukuba Mkoani Kigoma wanavyoweza kupata huduma za Intaneti kupitia mtandao wa Vodacom mara baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua rasmi huduma za Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto (mwenye kofia nyekundu) ni Mhandisi wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Adam Nyamgali.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiongea na wakazi wa kijiji cha Bukuba na vijiji jirani waliofika kushuhudia uzinduzi wa mnara wa mtandao wa Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine kutoka kuhsoto ni Mhandisi wa Vodacom Adam Nyamgali, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Renatus Mkasa na Kaimu Mkurgenzi Mtendaji wa Wilaya Malcelina Mbehoma. Kupatikana kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunatarajiwa kufungua ukurusa mpya wa maendeleo ya kiuchumi an kijamii kijijini hapo.
Mhandisi wa Vodacom Mkoani Kigoma Adam Nyamgali akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma jenereta inayozalisha umeme wa kuendeshea mnara wa mawasiliano wa kampuni hiyo. Mkuu huyo wa Wiayaa aliuzindua mnara huo uliopo kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.

Zaidi ya wakazi 17,000 wa kijiji cha Bukuba wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma kunufaika na huduma za mawasiliano ya simu za mkononi za mtandao wa Vodacom baada ya kampuni hiyo kuzindua rasmi huduma zake kijijini hapo.

KIuzinduliwa kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunawapa nafais wakazi hao walio pembezoni mwa wilaya mpya ya Buhigwe kuwa na uwezo na fursa ya kuboresha maisha yao kupitia simu za mkononi ikiwemo kuboresha usalama, kurahisisha biashara n.k.

Huduma hizo zimezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya .

Akziundua huduma hizo mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Wilaya Gishuli ameelezea matumaini yake ya namna ambavyo maisha ya wakazi hao yanavyoweza kuboreka ikiwemo suala la ulinzi, wepesi na tija kwenye kilimo,ufugaji na biashara.

Amesema jiografia ya kijiji hicho na Wilaya ya Buhigwe kwa ujumla inatoa ulazima wa kuwa na mawasiliano ya uhakika ili kuweza kuistawisha shughuli za kiuchumi hususan biashara ambazo ndio nguzo kuu ya maisha ya wakazi wa hapo.

Amesema  Bukuba ina kiwango kikubwa cha biashara ikihusisha mazo ya ndizi na mifugo ambapo soko kuu ni mikoa ya Tabora, Katavi na nchi jirani ya Burundi.

“Leo ni siku njema kwenu wakazi wa Bukuba kupata huduma za Vodacom zitakazowawezesha kuwa na uhakika wa mawasiliano na kuboresha shughuli zenu z akiuchumi na kijamii tofauti na ilivyokuwa hapo awali .”

Natambua kuwa malori yenye mikungu ya ndizi inatoka hapa kwenda Tabora, Katavi, Rukwa na nchi jirani ya Burundi tumieni mawasilano kupata raatifa za kimasoko ikiwemo aina ya wateja, bei na kiwango cha mahitaji ili kupunguza adha ya kusafirisha mzigo kwa kubahatisha soko, kwa njia hiyo sasa mnayo kila sababu ya kufanya biashara kwa ufanisi na tija zaidi.”

Aidha, amesema ujio wa Vodacom unaombatana na huduma ya M-pesa utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto zitokanazo na ukosefu wa huduma za kibenki kwenye kijiji hicho na eneo kubwa la wilaya hiyo mpya ya Buhgwe.

Amesema kupitia M-pesa ni wazi sasa benki zipo kwenye viganja vyao hivyo hawana sabbau ya kuwa na hofu ya kukosa huduma za kibenki kinachpaswa na kujifunza na kuitumia kwa ufasaha kwa maendeleo yao.

“Naamini mtatumia huduma ya M-pesa kuziba pengo la huduma za kibenki kwani kama tulivyoelezwa hapa kupitia M-pesa unaweza kuweka au kutoa fedha kutoka kwenye benki, hii ni nafasi yenu kuounguza gharama mlizokuwa mkiingia kufuata huduam za benki Wilayani Kasulu ama Kigoma Mjini.”

Amesema kwa wastanimakzi wa Bukuba anaekwenda mjini mara mbili au tatu kufuata huduma za benki humgharimua hadi Sh. 30,000 gharama ambayo kwa sasa wanaweza kuipeka na kutumia feha hizo katika shughuli nyengine.

Hata hivyo ametoa rai kwa Vodacom kushirikiana na benki zilzounganishwa na M-pesa kutoa elimu kwa wakazi hao ili waweze kunufaika vema hasa wafanyabaishara ambao wanalazimika kusafiri umbali mrefu na fedha.

Mkuu huyo wa Wilaya pia amezungumzia umuhimu wa Bukuba na Buhigwe kwa ujumla kuwa na huduam za uhakika za mawasiliano ili kuweza kukabiliana na changamoto za kiusalama hasa kutokana na kuwa mpakani.

“Wote tunajua changamoto za kiusalama ambazo maeneo yaliyo mipakani kama sisi yanavyokabiliana nayo, nawaomba tutumie mawasiliano haya ya simu ya mkononi kuongeza uimara wa usalama wetu na kwmaba sasa mnaweza hata kunipata kwa urahisi kutoa taarifa za viasharia vya matukio mabaya.”Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya

Gishuli akizungumzia umuhimu wa mawasiliano katika kuimarisha ulinzi na usalama, amesema ni jambo lililowazi kuwa uwepo wa mawasiliano ya uhakika kunaimarisha ulinzi hasa kwa wilaya kama ya Buhigwe iliyo mpakani.

Amesema mawasiliano ya uhakika yanaviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kupokea taarifa mbalimbali za uhalifu au viashiria vyake kutokana kwa wananchi au hata kubadilishana taarifa na wenao wa nchi jirani.

Amewataka wakazi hao kwa kuwa sasa wana uhakika wa mawasiliano kumpatia taarifa mara moja kupitia simu yake ambayo aliitaja hadharani huku akiiiomba pia Vodacom kuendelea kuimarisha huduma zake wilayani humo kwenye maeneo ambyo bado yana ukorofi.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akizungumza kwenye uzinduzi huo alisema usimikwaji wa huduma za Vodacom kijijini hapo ni mwendelezo wa mpango mkakati wake wa kuhakikisha inawaunganisha watanzania wakiwemo wa vijijini kwenye mtadao wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi.

Amesema Vodacom itaendelea  kutilia mkazo mpango huo ikiwemo kwenye maeneo yaliyo pembezoni kama Bukuba kwa kuwa Vodacom inaamini kuwawezesha wananchi kimawasiliano ni kuwapa fursa ya kubadili maisha yao.

"Mhe.Mkuu wa Wilaya, kazi iliyofanywa na Vodacom hapa Bukuba inafanyika pia sehemu mbalimbali za nchi kwa shabaha ya kuwaunganisha watanzania kwenye mtandao wa simu za mkononi.”Alisema Mwalim

“Ni Imani yetu kwmaba sasa maisha ya wakazi wa Bukuba yatabadilika, baishar zitakua zaidi na shughuli za kilimo zitaimarika zaidi ya ilivyokuwa hapo awali, matokeo ya haya yote ni kuboreka kwa maisha ya wananchi, hilo ndio lengo la Vodacom.”Aliongeza Mwalim

Mwalim amesema katika maisha ya sasa huduma za mawsiliano ya simu za mkononi sio tena anasa, kila mmoja anapaswa kufikiwa na huduma hiyo na kwmaba Vodacom itaendelea kuwaunganisha watanzania mijini na vijijini.

“Hatuangalii mijini tu, walio vijijini nao ni sehemu muhimu ya mikakati yetu tukitambua nao wana nafasi kubwa ya kuboresha maisha yao iwapo tutawapatia huduma zetu, kwetu sisi kila mmoja tunampa umuhimu na uwepo wetu Bukuba leo ni matokeo ya kile tunachokiamini na kukitekeleza.”Alisema

Aidha Mwalim amewakumbusha kujiunga na vifurushi vya Vodacom ikiwemo cha cheka ambavyo vinalenga kuwapatia watejahuduma bora na kwa gharama nafuu.

No comments: