Na Mwandishi Maalum
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, imesisitiza
kuwa, Mpango wa Utekelezaji kuhusu Idadi
ya watu na Maendeleo (ICPD) unapashwa kuzingatia pamoja na mambo mengine umalizaji
wa ajenda ambazo hazijakamilika au kwa maneno mengine
viporo vilivyobaki.
Tanzania imevitaja viporo hiyo kuwa ni upunguzaji wa umaskini, tofauti za usawa wa jinsia, elimu kwa watoto wa kike, uimarishaji wa huduma za afya, utokomezaji wa magonjwa mbalimbali yakiwamo malaria,
kifua kikuu na maambukizi ya virusi ya Ukimwi.
Msisitizo
huo wa Tanzania umetolewa na Bw. Charles
Pallangyo, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, katika siku ya tatu ya Mkutano wa 47 wa Tume ya Idadi ya Watu na Maendeleo, (ICPD)
unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa.
Katibu Mkuu
Pallangyo anaongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika Mkutano huo ambapo washiriki wanaoziwakilisha Serikali zao , wanafanya tathmini
ya hali ya utekelezaji wa Mpango
wa Utekelezaji wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Idadi ya Watu na Maendeleo uliofanyika miaka 20 iliyopita
huko Cairo, Misri.
“
Tanzania imejitahidi sana na imefanikiwa katika utekelezaji wa Mpango wa Cairo, yapo maeneo ambayo tunajivunia ,nayo ni, upunguzaji wa
idadi ya vifo vya watoto wachanga,
kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika ngazi za utoaji wa maamuzi kama vile
Bunge na taasisi nyingine, fursa
sawa za elimu kwa uwiano wa jinsia,
uwezeshwaji wa wanawake na haki
za binadamu kwa uchache” akasema katibu Mkuu na kuongeza.
Pamoja
na mafanikio hayo na mengine mengi, bado kuna maeneo ambayo mafanikio yake si ya kuridhisha sana. Baadhi ya maeneo hayo ni upunguzaji wa vifo vya wanawake wajawazito na
utokomezaji wa magonjwa kama vile maambukizi ya
virusi vinavyosababisha ukimwi.
“ Ni kwa sababu hiyo basi, sisi ( Tanzania) tunataka kutilia mkazo kwamba, kima ilivyokuwa miaka 20 iliyopita, ICPD ni muhimu sana hasa katika
maandalizi ya ajenda za maendeleo endelevu baada ya 2015. ni lazima pia kutilia mkazo utekelezaji
wa viporo ambayo havikumalizwa wakati wa
utekelezaji Malengo ya Maendeleo ya Millennia ambayo yanafikia ukingoni”
akasisitiza Katibu Mkuu Pallangyo.
Akaogeza
kwamba, Mpango wa Utekelezaji wa ICPD ni
vema pia ukashughulikia changamoto mpya zinazoibuka hivi sasa zikiwamo za
uongezeko la idadi ya wazee ,ongezeko
ambalo linapita idadi ya watoto wadogo chini ya miaka mitano.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, ni
kati ya nchi 47 zilizochaguliwa na Baraza Kuu la Uchumi na Ustawi wa Jamii (
ECOSOC) kuwa mjumbe wa Tume ya Idadi ya Watu na Maendeleo. Wajumbe hudumu wa katika Tume hiyo kwa kupindi cha miaka mine na huchaguliwa kwa mgawanyo wa kijiografia.
Pamoja na wajumbe wanaotoka serikali mbalimbali, mkutano huu unahudhuriwa pia na idadi kubwa
ya wajumbe kutoka Asasi zisizokuwa za kiserikali.
Kwa
mujibu wa taarifa mbalimbali zilizowasilishwa
wakati wa mkutano huu
zinazonyesha kwamba kwa ujumla kumekuwapo na mafanikio makubwa katika kipindi hicho cha miaka 20 tangu
kufanyika kwa mkutano huo wa Cairo mwaka 1994.
Baadhi
ya mafanikio hiyo ni kuongezea kwa umri
wa watu kuishi ambapo sasa dunia inasadikiwa kuwa na wazee wengi, kuongezea kwa
wakazi wa mijini, kupungua kwa vifo vya watoto wachanga, wanawake kujipatia
fursa ya kimiliki ardhi katika baadhi ya nchi,
Katika
Mkutano huo wa Kimataifa wa Cairo
ambao unatajwa kuwa ni mkutano wa kihistoria, uliohudhuriwa na nchi 179 ambazo ni wanachama wa Umoja wa
Mataifa ambapo mkazo ulikuwa kwamba binadamu ndiye mlengwa mkuu katika jitihada za kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii
Ni katika Mkutano huo ambapo suala la upatikaji wa huduma za elimu , afya na haki
za binadamu hasa wanawake na vijana kulielezwa
kama kungesaidia uchagizaji wa
maisha bora kiuchumi na kijamii na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo
endelevu na mwenendo endelevu wa idadi ya watu
Aidha wakati wa mkutano huo wajumbe walijiwekea
malengo ya utekelezaji katika maeneo ya
upunguzaji wa umaskini,
utokomezaji wa tofauti za kijinsia,
maendeleo ya miji na
uhamiaji, maendeleo ya
jamii, na haki za wanawake na vijana katika maeneo mbalimbali kama vile haki za afya pamoja na afya ya uzazi.
No comments:
Post a Comment