Katibu tawala wilaya ya Makete Joseph Chota ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Makete, akitoa hotuba kwa wananchi wa kijiji cha Isapulano
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Makete Dkt. Michael Gulaka akitoa taarifa ya chanjo kwa mgeni rasmi na wananchi waliofika Isapulano.
Mgeni rasmi akihutubia
Mgeni rasmi Joseph Chota akitoa chanjo kwa mtoto Sarafine Mahenge.
Mgeni rasmi akitoa chanjo kwa mtoto Horence Luvanda
Mgeni rasmi Joseph Chota akitoa chanjo kwa mtoto Elifata Tweve.
Kulia ni baba aliyeonesha mfano kwa kumleta mtoto wake wa kike kupata chanjo
Wananchi wakipanga foleni kwenda kuwapa watoto wao chanjo.
==============
Ubovu wa miundombinu ya barabara wakati wa masika katika wilaya ya Makete mkoani Njombe umeelezwa kuwa miongoni mwa vitu vinavyochangia huduma ya chanjo kutofika kwa wakati katika zahanati zinazotoa chanjo wilayani hapo.
Hayo yameebainishwa na Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya ya Makete Dkt. Michael Gulaka hii leo wakati akisoma taarifa ya idaya ya afya siku ya uzinduzi wa wiki ya chanjo iliyoadhimishwa kiwilaya katika Kata ya Isapulano wilayani Makete. Dkt Gulaka ametaja changamoto nyingine ni pamoja na zahanati za Utengule, Ugabwa na Igolwa bado hazitoi huduma ya chanjo kutokana na uchache wa wahudumu wa afya na upungufu wa wahudumu katika sekta ya afya.
"Unakuta zahanati inamtumishi mmoja hivyo anapokwenda likizo au kwenye mafunzo huduma za chanjo hazitolewi hivyo kuathiri kufikia kiwango kilichokusudiwa lakini si hilo tu wkati wa masika zahanati nyingi hazifikishiwi chanjo kwa wakati kutokana na ubovu wa barabara, magari hayafiki na wakati mwingine yanafika kwa tabu" amesema Dkt. Gulaka.
Akihutubia wanakijiji waliofika katika uzinduzi hao Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu tawala wilaya Bw. Joseph Chota kwa niaba ya mkuu wa wilaya amesema serikali imejipanga vilivyo kuimarisha huduma ya mkoba kwa maeneo yaliyombali na vituo vya kutolea huduma za afya, pamoja na kuendelea kuomba vibali vya kuajiri watumishi wapya wa afya kama njia mojawapo ya kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Bw. Chota amesisitiza wazazi na walezi kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo kwa wale ambao hawajakamilisha ili kupunguza magonjwa ambayo yanazuilika kwa watoto.
Katika hatua nyingine amesema kwa wilaya ya Makete kumekuwa na mwamko wa wanaume wengi kuamua wao wenyewe kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya kupatiwa chanjo tofauti na ilivyokuwa mwanzoni kuwa hilo ni jukumu la wanawake tu, na kusema kwa kufanya hivyo kutapelekea ushirikiano wa pamoja katika kumtunza mtoto wao.
Mgeni rasmi baada ya kuzindua wiki ya chanjo kiwilaya ambayo imeanza leo Aprili 24 - 30, pia ametoa chanjo kwa watoto watatu ambao ni Sarafine Mahenge, Horence Luvanda, na Elifata Tweve kama ishara ya uzinduzi rasmi na baada ya hapo wahudumu wa afya kuendelea kutoa chanjo kwa watoto wengine waliofika kwa ajili ya huduma hiyo
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Chanjo ni jukumu la wote"
Picha/Habari Edwin Moshi wa globu ya jamii kanda ya nyanda za juu kusini
No comments:
Post a Comment