Na Faustine Ruta, Bukoba
Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa kawaida kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku.
Awali akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua soka kwa ujumla nchini Tanzania na Kagera ikiwemo.
Katika mambo mengi aliyoeleza ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja, Lakini pia amehaidi kuitisha Harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Pia aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya Uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiudhuru nafasi hiyo, (Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiudhuru, Lakini kila mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiudhuru mpaka wengine kutamka kuwa iwapo nitajiuzuru basi nao watajiudhuru nafasi hii, lakini kuna mjumbe kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa sitojiudhuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi akizungumza na Wajumbe waliojitokeza katika mkutano huo wa Utekelezaji wa Chama cha Mpira wa Miguu (KRFA) Mkoa wa Kagera, Ambapo pia alizungumzia swala zima la kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku akizungumza na wajumbe
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi(kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku.
Kushoto ni Bw. Christopher Kiiza, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji KRFA - TFF KageraTaswira, Katika Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera, Ambapo mkutano huo ulifanyikia
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi(kushoto) akiwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku wakiteta jambo.
Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya utendaji TFF anayewakilisha Mikoa ya Kagera na Geita Bw. Kalilo Samson Kalilo. Akipitia Taarifa ya Utekelezaji Kamati ya Utendaji
Baadhi ya wajumbe wakipitia taarifa ya Utekelezaji ya Kamati ya Utendaji ya Chama cha mpira wa Miguu KRFA Mkoa wa Kagera
Mwenyekiti wa BUFA Bw. Marick Tibabimale (kushoto) na Kulia ni Bw. Jerome Simon
Mjumbe wa Kamati ya utendaji TFF anayewakilisha Mikoa ya Kagera na Geita Bw. Kalilo Samson Kalilo akizungumza na Wajumbe.
Mkurugenzi wa sheria TFF Evodius Mtawala akifafanua vipengele mbalimbali katika marekebisho ya Katiba ya KRFA.
Salum Hamis Umande Chama.
Muda wa kupata chakula cha mchana ulifika.
Viongozi wakiendelea kupata huduma ya chakula cha mchana kilichoandaliwa maalum kwa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera
wadau wa soka kwenye picha ya pamoja na Rais wa TFF bw. Jamal Emil Malinzi, kushoto ni Bw. Abdulzack na kulia ni Bw. Jamal Kalumuna
No comments:
Post a Comment